Saturday, February 11, 2017

Breaking News: Askofu Gwajima aachiwa kutoka polisi central jioni hii




Ni kutoka kwenye headlines za sakata la dawa za kulevya kupitia kwenye orodha aliyoitaja Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwenye awamu ya pili ambayo ilijumuisha majina ya watu 65 akiwemo Askofu Gwajima.

Kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam jioni hii, Askofu huyo wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwa anatoka kwenye kituo hicho cha Polisi alikokua ameshikiliwa toka Alhamisi kufuatia kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda.

Baadhi ya Waumini wa Kanisa lake walikua nje ya kituo hicho cha Polisi jioni hii na walisikika wakizungumza maneno mbalimbali ya kushukuru kama vile “Asante Yesu”


No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...