Sunday, February 12, 2017

Yanga yaitungika 5-1 Ngaya Moroni

Kikosi Cha Yanga





YANGA SC wameanza vizuri mawindo yao ya ubingwa wa Afrika, baada ya kwachapa wenyeji Ngaya Club de Mde mabao 5-1 jioni ya leo mjini Moroni, Comoro.


Ushindi huo unamaanisha Yanga watakuwa na shughuli nyepesi tu katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Dar es Salaam, kwani hata wakifungwa 3-0 watasonga mbele.


Kiungo Mzambia, Justin Zulu alifungua akaunti yake ya mabao Jangwani baada ya kusajiliwa msimu huu kwa kuifungia Yanga bao la kwanza dakika ya 43.




Kikosi cha Yanga kilichoanza leo Moroni na kuwachapa wenyeji 5-1


Winga machachari, Simon Happygod Msuva akaifungia Yanga bao la pili dakika ya 45 na Yanga ikaenda kupumzika inaongoza kwa mabao 2-0.


Mzambia mwingine, Obrey Chirwa akaifungia Yanga bao la tatu dakika ya 59, kabla ya Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe kufunga la nne dakika ya 65 na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kufunga la tabo dakika ya 73.


Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi dakika ya 66 kupitia kwa Said Anfane Bourah Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.


Kikosi cha Ngaya kilikuwa; Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir, Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana Falinurina na Chadhuili Mradabi.


Yanga SC; Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Maka


No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...