Wednesday, February 1, 2017

UFAFANUZI: Ni kweli Ridhiwani Kikwete alichukia Diamond kupewa Bendera? alimaanisha nini?


Mwimbaji Mtanzania Diamond Platnumz alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa michezo na sanaaNape Nnauye baada ya kualikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya soka ya Afrika 2017 kwenye taifa la Gabon.

Baada ya hapo Ridhiwani aliandika kuhusu timu ya taifa ya soka ambapo wengine waliitafsiri post yake kama amechukia Diamond kupewa bendera lakini leo kupitia The Beauty TV amehojiwa na kutoa ufafanuzi.

Kwanza watu wanatakiwa kuelewa kwamba ile post haikuwa kwasababu ya Diamond na hata ukisoma kwenye maandishi yangu hakuna sehemu Diamond ametajwa isipokua msg iliyo pale inaweza kuwa inamgusa Diamond‘ – Ridhiwani

Kilichonifanya niandike ile msg ni ule wivu wa kuona kwamba mashindano yanayokwenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu lakini kilichotushangaza badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu tunawapa Waburudishaji kina Diamond

Matarajio yetu sisi watu wa mpira ni kuona Nahodha wa timu ya taifa akipokea Bendera, aliyepaswa kupokea bendera ni captain wa timu ya taifa……. hii pia lakini ni kuwapa changamoto TFF, je wao wanashangilia kuona Diamond amepewa bendera?

Mtazamo wangu mkubwa ulijikita huko na sio mtazamo wa kwamba Diamond sijui nani………. NO NO… Diamond yeye nampongeza sana kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri na ndio maana watu wamemuona wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza lakini kikubwa ni nini ajenda kubwa Gabon? ajenda ni mpira wa miguu‘ – Ridhiwani Kikwete

Diamond sio mcheza mpira wa miguu, hata kama anashabiki atakua ni mshabiki tu…. sisi kama Mashabiki  wa soka tunaona wenzetu wanajiandaa kuhakikisha timu zao zinafuzu kwenda kucheza katika hatua ile, sisi kwetu tunaandaa Wanamuziki kwenda kuburudisha, ni jambo la kusikitisha sana’ – Ridhiwani

No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...