Monday, September 18, 2023

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

 


Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbwa na mafuriko makubwa ya mashariki mwa nchi hiyo.


Jumapili iliyopita, kimbunga cha “Daniel” kilipiga maeneo kadhaa mashariki mwa Libya, na hasa hasa miji ya Benghazi, Al-Bayda, Marj, Susa, Shahatt na Derna.


Baada ya kimbunga hicho, Shirika la Afya Duniani lilionya kuhusu kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga na mafuriko hayo.


Kwa mujibu wa shirika la habari la IRIB, Haidar al-Sayeh, mkuu wa Kituo cha Taifa cha Kudhibiti Magonjwa nchini Libya, alitoa taarifa na kutangaza idadi ya sumu ambazo zimeripotiwa kutokana na matumizi ya maji ya kunywa huko Derna, Libya.


Akizungumzia kutotumika maji ya kunywa katika jiji la Derna, Al-Sayeh amesema kuwa, hali ya hatari ya mwaka mmoja itatangazwa katika maeneo yaliyoathiriwa na dhoruba na mafuriko mashariki mwa Libya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wowote wa kuambukiza katika maeneo haya.


Shirika la Afya Duniani lilitangaza siku ya Jumamosi kuwa, zaidi ya watu 9,000 wametoweka katika mji wa Derna mashariki mwa Libya.


Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga hicho nchini Libya hadi sasa imetangazwa kuwa zaidi ya 11,000.

Taiwan yanasa ndege 103 za kivita za China kwenye anga yake



 Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, idadi kubwa isiyo kawaida.


Kati ya Septemba 17 na 18 asubuhi, Wizara ya Ulinzi imenasa jumla ya ndege 103 za China, ikiwa ni rekodi katika kipindi cha hivi karibuni na inaleta matatizo makubwa ya usalama katika pande zote za mlango wa bahari wa Taiwan na katika kanda,” wizara imesema katika taarifa yake.


“Uchochezi wa kijeshi unaoendelea” kutoka Uchina “unaweza kusababisha kuongezeka kwa mvutano na kuzorota kwa usalama katika eneo hilo,” imeonya wizara hiyo, ambayo inaitaka Beijing “kukomesha mara moja vitendo hivi vya uharibifu vya upande mmoja.”


Kati ya idadi ya ndege za kijeshi zilizonaswa, 40 zilivuka mstari wa wastani – mpaka usio rasmi kati ya China na Taiwan ambao China haitambui – na kuingia katika zili katika eneo la utambulisho wa ulinzi wa anga wa kusini (Adiz) -magharibi na kusini mashariki, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari. Meli tisa za kivita za China pia zilionekana karibu na kisiwa hicho

Askari wa kike Tanzania washiriki mkutano wa mwaka 2023 New Zealand

 Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wameshiriki mkutano wa mwaka 2023 wa mtandao wa polisi wanawake duniani (IAWP) nchini New Zealand.



Mkutano huo umebeba kaulimbiu isemayo” Refresh, Renew,Refocus umefunguliwa September 17,2023 mji wa Auckland.





Aidha Mkutano huo umeudhuriwa na mataifa 65 yakiwemo mataifa mengine kutoka Afrika kama vile Tanzania,Ghana na Africa Kusini.





Itakumbukwa mwishoni mwa mwezi Julai Tanzania ilikuwa mwenyeji wa mkutano kama huo kwa ukanda ya Afrika uliyofanyika jijini Dar es salaam na kuleta matokeo makubwa ya kiutendaji kwa maafisa na askari wa kike ambao walishiriki na mada mbalimbali kufundishwa lengo likiwa kuwaongezea uwezo na maarifa ya kiutendaji.





Mkutano huo uliofunguliwa leo septemba 17,2023 katika mji Auckland Nchini New zealand unaoambatana na mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wa kike, sambamba na kutoa fursa na kutengeneza mtandao wa mawasiliano kwa wasimamizi wa sheria.





Mbali na hilo Ujumbe huo kutoka Tanzania uliongozwa na Kamishna wa Polisi CP Suzan Kaganda wa kamisheni ya Utawala na rasilimali watu umetumia mkutano huo kutangaza utalii na vivutio vya kitamaduni vilivyopo Tanzania.



Mkutano huo hutahitimishwa Septemba 21,Mwaka huu.



Urusi yazuia mashambulizi mapya ya ndege zisizo na rubani za Ukraine

 


Urusi imedai kuangusha ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine katika eneo lililokaliwa la Crimea, katika mkoa wa Moscow pamoja na ile ya Belgorod na Voronezh, karibu na Ukraine.


Ndege kadhaa ziliharibiwa katika eneo lililounganishwa la Crimea, katika mkoa wa Moscow na ile ya Belgorod na Voronezh, usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu.


“Drones zilinaswa juu ya maeneo ya magharibi, kusini-magharibi, kaskazini-magharibi na mashariki mwa peninsula ya Crimea, Istra (magharibi) na Domodedovo (kusini) wilaya za mkoa wa Moscow, mikoa ya Belgorod na Voronezh (kusini-magharibi),” Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema kwenye Telegramu, bila kubainisha idadi ya ndege zilizoharibiwa au kuripoti uharibifu au majeruhi kufikia hatua hii.


“Vituo vya uzalishaji wa kiwanda cha kivita cha Kharkiv, ambapo ukarabati na utunzaji wa magari ya kivita ya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine ulikuw ukifanyika, vlipigwa na mashambulizi haya anga,” chanzo hicho pia kimetangaza.


Hapo awali, mkuu wa utawala wa jeshi la Ukraine, Oleg Synegubov, aliripoti kwenye Telegram kwamba moja ya makampuni katika jiji hilo ilipigwa na “makombora manne ya S-300” na moto ukazuka.

WATAKAO TUPA TAKA HOVYO NJOMBE MJINI KUCHUKULIWA HATUA KALI


Katika kuadhimisha siku ya Usafishaji Duniani Septemba 16,2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Ndugu Kuruthum Sadick amesema Halmashauri haitamvumilia mwananchi yeyote, atakayeonekana kuchafua mazingira kwa kutupa taka hovyo mitaani na kwenye maeneo yasiyo rasmi.


Akielezea umuhimu wa usafi na kutunza mazingira Mkurugenzi Kuruthum amesema kuwa, usafi ni afya na ukitunza mazingira yanakutunza hivyo kila mwananchi anawajibu wakuhakikisha anafanya usafi kwenye maeneo yanayomzunguka kutunza maeneo ya mabonde na vyanzo vya maji kwa kuacha kutupa takataka hovyo.


Akiwa eneo la bonde linalopita mtaa wa National Housing kata ya Njombe Mjini ,ametoa onyo kwa wananchi ambao wanatupa taka kwenye bonde hilo ambalo siyo dampo rasmi kwa ajili ya takataka nakusema Halmashauri imetenga eneo rasmi kwa ajili ya kutupa taka hivyo bonde hilo lisitumike kutupia taka.


“Tumeweza kujumuika kufanya usafi kwenye hili bonde ni wasihi wananchi kuacha kutupa taka kwenye bonde hili na yeyote atakayebainika hatua kali zitachukuliwa,na tufahamu kuwa kuna vyanzo vyanzo vya maji kwenye bonde hili na tunaelekea msimu wa mvua siyo afya kwa vyanzo vyetu vya maji maana maji haya yanatumika, Halmashauri ina magari yakukusanya taka kupeleka dampo tuache kabisa kutupa taka kwenye eneo hili ambalo siyo rasmi ”


Katika hatua nyingine amesema ili kuhakisha Mji wa Njombe unaendelea kubaki katika hali ya usafi ,Halmashauri ya Mji Njombe itaendelea kuhamasisha na kushiriki usafi wa pamoja kila mwezi ili kuwa kumbusha wananchi kuwa wanawajibu wakutunza mazingira na kufanya usafi mpaka kwenye maeneo yanayowazunguka majumbani.


“Usafi usiishie hapa tu,tufanye usafi hadi majumbani, hii itatukinga na magonjwa, kama kipindupindu”


Kwa upande wake Afisa Afya wa Mkoa wa Njombe Bi.Saada Milanzi amesema ili kuendelea kutunza mazingira Halmashauri zote za mkoa wa Njombe ziendelee kutumia sheria ndogo zilizopitishwa ili kuwawajibisha na kudhibiti utupaji taka kwenye maeneo yasiyo rasmi.


Aidha ametoa wito kwa wananchi kuitikia wito wakushishiriki shughuli za usafi na kutii sheria mbalimbali za usafi na utunzaji wa mazingira zilizowekwa na Halmashauri ili kuweka mazingira safi na kuzuia magonjwa ya mlipuko .


Naye mtendaji wa kata ya Njombe Mjini Enos Lupimo ameeleza mikakati waliyonayo katika kuweka eneo la Mji safi pamoja na kupambana na utupaji wa taka hovyo kwenye maeneo yasiyo rasmi kama kwenye mabonde.


“Sisi kama kata tunaenda kuunda kikosi kazi ambacho kitafanya kazi kuanzia ngazi ya mtaa ,kitahusu mazingira na afya,tutaoa elimu ya usafi na utunzaji wa mazingira na kisha tutaanza kuchukulia hatua wananchi ambao watakiuka sheria nakutupa taka hovyo kwenye mabonde na mitaani,tutakuwa na walinzi kwenye haya mabonde watafanya kazi usiku na mchana ,na ukionekana unatupa taka hovyo faini itahusika kwa mujibu wa sheria”.


Wadau mbalimbali ambao wameshiriki kuadhimisha siku hii ikiwemo taasisi ya SHIPO , Benki ya Taifa ya Uchumi (NBC),wanafunzi pamoja na vikundi vya vijana vinavyojishughulisha na mazingira ,wamesema jamii inatakiwa kutambua kuwa taka ni mali hivyo wanaweza kuzikusanya kwa utaratibu wakuzitenga taka ngumu zisizooza kama vile chupa za plastiki na zikatumika kwenye utengenezaji wa bidhaa mbalimbali.


Halmashauri ya Mji Njombe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na wananchi imeungana na nchi mbalimbali Duniani kuadhimisha siku ya usafishaji duniani kwa kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe .

Sunday, May 27, 2018

KINGS FM TOP 30 MAY 27 KWA NGWARU BADO NI SHEEEDAH


Midundo mikali inasikika kila kona kwenye media tofauti tofauti duniani kote, Nchini Tanzania Media nyingi zimekuwa zikitumia siku za weekendy (Jumamosi na Jumapili) katika kuwasilisha Ngoma mbalimbali ambazo zinafanya poa katika chart kama Top 10, Top 20 na Top 30.

KINGS FM TOP 30 (01-15)

Kupitia Kings Fm Radio 104.3MHz Njombe Tz Radio ambayo pia waweza isikiliza kupitia king'amuzi cha Azam Tv Channel no 055 au kwa kupakua app ya Kings FM Radio kupitia simu yako ya Android (www.kingsfm.co.tz) hizi ndizo ngoma 30 kali kwenye Chart ya KINGS FM TOP 30.
KINGS FM TOP 30 (16-30)


Mpango mzima unaletwa kwenye redio yako Chini ya Lizrome Pouline chart imepangwa chini ya usimamizi wa Idara ya Muziki ikiongozwa na Teja wa Muziki Josee M'bongo, Sikiliza kuanzia saa 1200 - 1500 mchana.

Thursday, April 5, 2018

ZILIZOBAMBA



1. Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amezungumzia sababu za kukosekana kwa hotuba yake Bungeni na kusema Wamegomea Kusoma Hotuba Za Kambi Hiyo Kwa Wizara Yoyote Mpaka Watumishi Wa Ofisi Hiyo Watakaporejeshwa Kazini.
Freeman Mbowe

2. Moja kati ya stori inayoshika headlines kutoka nchini Libya ni hii kutoka Mahakama ya Tripoli ambayo imefuta kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili Saadi Gaddafi, mtoto wa tatu wa aliekua rais wa Libya, Muammar Gaddafi.

Saadi Kaddafi amefutiwa mashtaka yote dhidi yake katika kesi ya mwanamichezo Bachir al-Rayani ambaye alifariki dunia mwaka 2006 baada ya kupigwa kichwani, Bachir Rayani alifariki dunia baada ya malumbano katika nyumba inayomilikiwa na Saadi Gaddafi.

3. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa uamuzi April 23,2018 kuhusu kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili mrembo Wema Sepetu na wenzake kama wana kesi ya kujibu au hapana na uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashtaka.

Mbali na Wema washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina Msigwa  na Matrida Seleman Abbas.
Wema Sepetu


4. wasanii wengi kutoka Zanzibar wamekuwa waisahau fadhila na kusahau walikotoka hasa pale wanapohamishia majukumu yao kikazi Jijini Dar es Salaam, huyu hapa ni nedy music kutoka Zanzibar hapa anawajibu mashabiki wake ambao wanasema amekusahau kabisa Zanzibar.
Nedy Music

5. Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka Watanzania wawe wepesi wa kutoa pongezi pale wasanii wa filamu nchini Tanzania wanapofanya vizuri, na sio kuwabeza na kuwaponda kila siku kwani kitendo hicho kinawakatisha tamaa waigizaji wetu.
Haji Manara

Via ➡KingsFmRadio 104.3Mhz
      ➡KingsFmRadioAndroidApp 
      ➡Tunnein 12:00-12:15 pm
         www.kingsfm.co.tz

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...