Saturday, February 4, 2017

MIX Tundaman kayaandika haya baada ya ‘Tunda’ kutajwa kwenye list ya Mh. Makonda



 Tunda Man ni msanii wa bongofleva ambaye makazi yake ni Dar es salaam ambapo February 3 2017 Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda alizungumza kwenye makao ya Polisi kituo cha kati na kusema miongoni mwa watu atakaowahitaji wakamuone Jumatatu kwa ishu ya dawa za kulevya ni pamoja na Tunda.

Kwa sababu mkuu wa mkoa hakutumia majina halisi ya kuzaliwa, watu mbalimbali walianza kumpigia simu msanii Tunda Man baada ya kuambiwa jina lililotajwa na Makonda ni Tunda.

Baada ya simu za kutosha Tunda Man aliamua kuandika Instagram kwamba sio yeye aliyetajwa bali aliyetajwa ndio huyo kwenye picha, akaambatanisha na picha ya Mrembo Tunda ambaye ameonekana kama video queen kwenye video za bongofleva.

Tundaman aliandika ‘Jamani Tunda aliyetajwa na Muheshimiwa @PaulMakonda ni huyu na sio mie maana simu zimekua nyingi, @Sudibrown na wewe hujui au umeamua kunipigia tu….’



No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...