Dodoma. Siku chache baada ya wabunge kueleza kutoridhishwa na Serikali kuhamia kwenye majengo ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii nayo imepinga hatua hiyo.Kamati hiyo pia imeshauri Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), kuachana na utaratibu wa kupangia wanafunzi vyuo na ijikite kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na vyuo vikuu nchini.
Mapendekezo hayo yalitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2016.
Wizara ambazo zimehamishia ofisi zake Udom kutoka Dar es Salaam ni Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Katiba na Sheria; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. #Mwananchi
Monday, February 6, 2017
WABUNGE WAPINGA WIZARA KUTUMIA MAJENGO YA CHUO CHA UDOM.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New Posts
Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko
Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...
-
.Na.Ahmad Mmow. Mahakama ya mkoa wa Lindi,leo imewachia huru makada watatu wa CHADEMA waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la kushiwishi kute...
-
KINGS FM TOP 30 MAY 27 KWA NGWARU BADO NI SHEEEDAH Midundo mikali inasikika kila kona kwenye media tofauti tofauti duniani kote, Nchin...
-
1. Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amezungumzia sababu za kukosekana kwa hotuba yake Bungeni na kusema Wame...
No comments:
Post a Comment