Wednesday, February 8, 2017

Wema Sepetu Apelekwa Kupimwa Kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Kujua Kama Anatumia Madaw Au Lah.



Taarifa zilizotufikia zimeeleza kuwa, msanii wa Bongo Movie, Wema Sepetu hajafikishwa mahakamani Kisutu leo kwa madai kuwa amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwa ajili ya kupimwa na kuthibitisha  iwapo anatumia madawa ya kulevya au la!

Imedaiwa kuwa, Polisi Dar, wamefikia hatua hiyo baada Wema kukana kutumia madawa wakati alipokuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Taarifa zimedai kuwa mastaa wenzake kama TID na wengine walikiri kutumia madawa na kupewa onyo kali huku mahakama ikiwapa masharti matatu likiwemo la kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja na kuwa chini ya uangalizi wa mahakama, kisha kujidhamini kwa bondi ya shilingi milioni moja na kurudi uraiani wakati Wema akikana kutumia madawa.

Taarifa zaidi zimedai kuwa, polisi wanaendelea kumshikilia Wema huku wakisubiri ripoti ya mkemia mkuu ili waweze kukamilisha upelezi na kumchukulia hatua zinazostahili.


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...