Mkuu wa mkoa wa Dar es salaamPaul Makonda leo February 8 2017 ametangaza kuiachia orodha ya Watu 65 wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo amemtaja pia Mbowe ndani yake.
Dakika chache baada ya kumtaja,CHADEMA Makao makuu Dar es salaam walikutana na Waandishi wa habari na kusema yafuatayo >>> “Kimsingi katika majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, swala la utetezi wake au maelezo hilo ni swala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani“
“Tunalaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria, Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita“
‘Kitendo cha kwenda kuongea kwenye mkutano na Waandishi wa habari na kutaja viongozi wakuu wa kitaifa ambao wana tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa, ni kukosa ustaarabu wa kiuongozi… tusingependa kuona viongozi wengine Waandamizi kutendewa kama alivyotendewa kiongozi wa chama chetu“
Wednesday, February 8, 2017
CHADEMA mchana huu baada ya jina "Mbowe" kutajwa kwenye orodha ya Makonda
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New Posts
IJUE SCANIA P380[Mende]
Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...
-
Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...
-
Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, ida...
-
Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wameshiriki mkutano wa mwaka 2023 wa mtandao wa polisi wanawake duniani (IAWP) nchini New Zealand. Mk...
No comments:
Post a Comment