Friday, February 10, 2017

Mbowe: Siendi polisi kwa wito wa Makonda

Mbowe Akizunguza na Waandishi wa habari


RC hana mamlaka ya kisheria ya kumuita mtu Polisi, nitamfungulia mashtaka ya kunichafulia jina langu kwa kunihusisha na biashara ya dawa za kulevya, nipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote endapo njia sahihi zitatumika.

Mbowe ameyasema haya wakati akizungumza na waandishi wa habari


Sisi kama Chama tunaunga mkono jitihada za mapambano dhidi ya dawa za kulevya, Serikali imechelewa kuendesha vita, CHADEMA na Kambi ya Upinzani kwa ujumla haiungi mkono mapambano hayo yanayoendeshwa kwa hila.

RC anachofanya ni kuwaepusha watuhumiwa wa dawa za kulevya na mkono wa sheria.

Sjawahi kujihusisha kwa kufanya biashara wala kutumia madawa ya kulevya wakati wowote katika maisha yangu.


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...