Thursday, February 2, 2017

Sihusiki na madawa ya kulevya - Ditto



Msanii Lameck Ditto ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Moyo sikuma damu' amefunguka na kusema yeye hausiki na biashara ya dawa za kulevya wala matumizi ya dawa za kulevya na kusema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amekosea kutaja jina.

Lameck Ditto akiongea na EATV amesema kuwa hata yeye amesikia jina lake likitajwa kwenye kundi la wasanii ambao wanahitajika kufika kesho kituo cha polisi na kusema anadhani kuwa Mkuu wa Mkoa alikosea kutaja jina lake.

"Kiukweli mimi mwenyewe nimeshtuka sana maana sijihusishi kwa namna yoyote na madawa ya kulevya, siuzi wala kutumia na siku zote nayapiga vita sababu natambua si mazuri katika jamii, nadhani Mhe. alikosea kutaja jina maana alisema Ditto lakini baadaye niliona amerekebisha na kusema Titto, hivyo naomba Watanzania watambue mimi sihusiki na madawa ya kulevya" alisema Lameck Ditto


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...