Vanessa Mdee
Msanii wa muziki wa bongo fleva Vanessa Mdee ambaye kwa sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Cash Madame' amefunguka na kutoa siri ya kitu kinachomfanya kuwa bora na kufanikiwa kuwa ni pamoja na kufanya kazi sana na kuheshimu ratiba yake.
Akiongea kwenye kipindi cha 'Wanawake Live' kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana EATV Vanessa anadai kuwa huwa anapanga malengo ya kila kitu katika maisha yake, kuanzia kwenye kazi yake ya muziki na maisha ya kila siku.
"Nina malengo ya kila kitu, malengo ya pesa, muziki, malengo ya muziki video, na malengo ya watu wangapi wa kuongeza Instagram, hivyo na malengo ya kila kitu na nisipotimiza huwa inaniumiza sana kichwa changu. Mimi napiga kazi kama kichaa yaani hapa naondoka naenda studio, yaani kuna vitu huwa najiwekea lazima nivitimize ndani ya muda niliojiwekea, mfano kuwekeza kwenye ardhi, kuwekeza kwenye nyumba nayo jenga, na chochote nachotaka kukitimiza lazima nikiweke kwenye ratiba yangu" alisema Vanessa
Mbali na hilo Vanessa Mdee alitoa ushauri kwa watu kuwa ukitaka kufanikiwa kwa jambo lako licha ya mipango yako unapaswa kumtanguliza Mungu kwa kila jambo lako
"Kwanza mimi namtanguliza Mungu kwa kila kitu lakini pia sala au ibada bila kazi haviendani kwa hiyo mimi napanga ratiba ya kazi yangu kila siku kama saizi hapa nimepanga ratiba mpaka mwezi wa nne, kwa hiyo najua kila kitu nilichopanga kufanya ndani ya muda huu" alisema Vanessa.
No comments:
Post a Comment