Monday, February 6, 2017

WABUNGE WAPINGA WIZARA KUTUMIA MAJENGO YA CHUO CHA UDOM.

Majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)


Dodoma. Siku chache baada ya wabunge kueleza kutoridhishwa na Serikali kuhamia kwenye majengo ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom), Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii nayo imepinga hatua hiyo.Kamati hiyo pia imeshauri Tume ya Vyuo Vikuu (TCU), kuachana na utaratibu wa kupangia wanafunzi vyuo na ijikite kusimamia ubora wa elimu inayotolewa na vyuo vikuu nchini.

Mapendekezo hayo yalitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo kwa mwaka 2016.

Wizara ambazo zimehamishia ofisi zake Udom kutoka Dar es Salaam ni Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora; Katiba na Sheria; Kilimo, Mifugo na Uvuvi; Mambo ya Ndani ya Nchi na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. #Mwananchi


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...