_______________________________________
ASKARI wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Sajini John Komba na wenzake wanne wakiwemo mgambo na wanafunzi wa jijini hapa, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga kwa kosa la kusababisha kifo cha aliyekuwa kondakta wa daladala inayosafiri kati ya Nguvumali na Raskazoni, Salim Kassim (18) mkazi wa Mwamboni.
Wakili wa Serikali, Donata Kazungu akisoma shitaka hilo la mauaji linalowakabili watuhumiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hilda Lyatuu alisema Januari 26, mwaka huu katika Kambi ya JWTZ iliyoko Kata ya Nguvumali jijini Tanga, Komba mwenye namba MT 69500 na wenzake watatu walimuua Kassim katika eneo la kambi hiyo.
Wakili Kazungu aliwataja washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Adam Juma (20), Sofia John (20) ambao ni mwanafunzi, Yohana Warioba na Bernard Nicholaus ambao ni wanamgambo wanaolinda katika kambi hiyo.
Hata hivyo, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Aidha, upelelezi kuhusu kesi hiyo haujakamilika na hivyo itatajwa tena Februari 26, mwaka huu. #HabariLeo
Monday, February 6, 2017
ASKARI JWTZ KIZIMBANI DHIDI YA KESI YA KIFO CHA KONDAKTA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New Posts
IJUE SCANIA P380[Mende]
Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...
-
Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...
-
Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, ida...
-
Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wameshiriki mkutano wa mwaka 2023 wa mtandao wa polisi wanawake duniani (IAWP) nchini New Zealand. Mk...
No comments:
Post a Comment