Tuesday, February 7, 2017

Zitto Kabwe Acharuka Kukamatwa Kwa Tundu Lissu;




" Kumekuwa na tabia ya kukamata Wabunge sasa hivi huyu Ndugu Lissu ni Mbunge wa pili ( wa kwanza alikuwa Mh Lema wa Arusha Mjini ). Sheria ya Bunge namba 3 ya 1988 sehemu ya 11 inakataza kabisa kumkamata Mbunge bila kutoa taarifa kwa Spika na desturi za Mabunge ya Jumuiya ya Madola zinakataa.
Tulitaka mjadala ndani ya Bunge ili Bunge liweze kuazimia kwamba mamlaka yoyote inapotaka kumkamata Mbunge imtaarifu Spika na Spika alitaarifu Bunge.

Naibu Spika hakukubali hilo, hivyo tumetoka hili kuprotest maamuzi hayo ya Naibu Spika. Na Wabunge kesho watarudi ndani ya Bunge ili kutaka maelezo  ya ziada kutoka kwa Spika mwenyewe kwamba ni kwa nini hadhi ya Bunge haizingatiwi kwa kiwango hiki "

Ndugu zitto kabwe ameyaeleza hayo muda mfupi alipozungumza na kipindi cha Jahazi cha clouds fm kwa njia ya simu


Mcheki Zito kabwe akizungumza Bungeni Dodoma Kuhusu suala la wabunge kukamatwa.


Zito Kwabwe


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...