Familia ya Jay Z na Beyonce inatarajiwa kukua zaidi hivi karibuni. Beyonce ametangaza kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa ni mjamzito wa watoto mapacha.
Hiyo ni habari njema kwa mashabiki wa familia hiyo ambayo miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiripotiwa kuwa na matatizo ya ndoa.
Beyonce ameandika:
We would like to share our love and happiness. We have been blessed two times over. We are incredibly grateful that our family will be growing by two, and we thank you for your well wishes. – The Carters
Tayari wawili hao wana mtoto wa kike mwenye miaka mitano, Blue Ivy.
Rihanna ni miongoni mwa mastaa waliompongeza Beyonce baada ya kutangaza habari hizo.
“So excited about this news!!!! Congratulations to you @beyonce and my big bro Jay!!!! 👼🏾👼🏾,” ameandika kwenye Instagram.
No comments:
Post a Comment