Wednesday, February 8, 2017

MSUKUMA APINGANA NA MAKONDA, ATAKA MALI ZAKE ZICHUNGUZWE

Mh. Paul Makonda


_____________________________________________

Vita iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ya kupambana na biashara ya madawa ya kulevya , sasa inaanza kuonekana kumgeukia kwa kukamiwa na baadhi ya wabunge.

Mbunge wa Geita vijijini , Joseph Msukuma(CCM), amedai kuwa Makonda anamiliki mali nyingi zisizoendana na muda aliokaa kwenye utumishi wa umma. ”Mh. Naibu Spika, RC wa Dar es salaam mwaka 2015 alikuwa akiishi kwa Membe, lakini tangu awe RC kwa mwaka mmoja sasa anatumia Lexus yenye thamani ya milioni 400, anamiliki V8 na mwanza amejenga maghorofa ndani ya mwaka mmoja,”amesema Msukuma.

Hata hivyo, Msukuma ametoa kauli hiyo ikiwa ni muendelezo wa kumtuhumu Makonda baada ya kufanya hivyo bungeni juzi aliposema anashangaa kuona Taifa linafanyia kazi taarifa ya Mkuu huyo wa Mkoa juu ya wauza dawa za kulevya.
#Lakefm


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...