Wednesday, February 1, 2017

Ngoma Ajiunga Na Wenzake Leo, Fiti Kuwavaa Stand United Ijumaa

Klabu ya Yanga imeendelea na mazoezi yake leo kwenye viwanja vya Chuo cha Polisi Kilwa Road huku Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe Donald Ngoma akirejea kujiunga na wenzake.

Mshambuliaji huyo ameanza mazoezi rasmi leo na kujiunga na wenzake baada ya kuwa nje kwa takribani mwezi m moja pamoja na kupata matatizo ya kifamilia ya kufiwa na kaka yake aliyekuwa anaugua ugonjwa wa kansa.

Ngoma aliyeumia goti kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi aliweza kukosa michuano hiyo kuanzia mchezo waio dhidi ya Zimamoto na pindi alivyorejea alitakiwa kukaa nje kwa wiki zisizopungua sita.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa Ngoma ameungana na wenzake leo na tayari ameanza nao mazoezi ya pamoja na hivi karibuni atarejea uwanjani.

Saleh amesema kuwa, Kocha Mkuu George Lwandamina aanaweza kumtumia katika mchezo unaofuata dhidi ya Stand siku ya Ijumaa kwani yuko fiti kwa sasa.  Andrew Vicent 'Dante' ameanza pia mazoezi na wenzake na mwalimu anaweza kumtumia kwenye mchezo ujao wa ligi kuu.

"Malimi Busungu ndiye hajaweza kuungana na wenzake kwakuwa alikuw ana malaria kali na alikuwa amelazwa sema kwa sasa ametoka anaendelea vizuri,"amesema Saleh.

Yanga wanakutana na Stand United huku wakitaka kuhakikisha wanatoka na ushindi ili kuendelea kuongoza ligi na kutetea ubingwa wao. Kikosi hicho kinaingia kambini baada ya mazoezi ya kesho asubuhi.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...