Wednesday, February 1, 2017

Ray C adai anarudi kwenye muziki kwa kasi baada ya watu kuonyesha wanavyomkubali

Baada ya ya kutumbuiza kwa mafanikio katika kikao cha Kamati ya Ushauri cha Mkoa wa Dodoma (RCC) juzi, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameweka wazi kwamba yupo mbioni kurudi upya katika muziki wa ushindani kwa kuwa anaamini bado muziki wake una mashabiki wa kutosha.

Ray C hayo baada ya kumaliza kutumbuiza nyimbo zake katika kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Mara baada ya kupanda jukwaani, Ray C alianza kuimba nyimbo zake za zamani huku vingozi mbalimbali wakijumuika naye kwa kucheza.

“Narudi kwa kasi, kama ulivyoona watu bado wananikubali, hayo mengine Mungu anasaidia naendelea vizuri,’’ alisema Ray C,” aliliambia Gazeti la Mtanzania.

Hata hivyo, Ray C, alisema kwamba kwa sasa ameshaachana na matumizi ya dawa za kulevya na lengo lake kubwa ni kurudi katika biashara yake ya muziki kutokana na kuendelea kukubalika kwa nyimbo zake.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...