Sunday, February 5, 2017

Mtanzania Na Mzambia Wadakwa India Na Mzigo Wa "Unga" Kilo Nne



Kushoto ni Mtanzania aliyejulikana kwa jina la Pamela David Kirrita (41) akiwa na mwanamke mwingine raia wa Zambia Thelma Mkandawire (38) wakiwa mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na kilo 4 za madawa ya kulevya aina ya cocaine katika hoteli moja kusini mwa jiji la New Delhi, India.

Naibu Mkurugenzi  Mkuu wa kikosi cha kupambana na madawa ya kulevya cha New Delhi (NCB)  Rajinder Pal Singh amesema watuhumiwa walikamatwa katika hoteli iliyo eneo la Mahipalpur jana Februari 4, 2017.

“Baada ya kupata taarifa kutoka vyanzo vyetu, timu yetu ikatega mtego kwa Mkandawire aliyewasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Indira Ghandi akitokea ughaibuni akiwa na mzigo huo.

“Baada ya kuchekiwa uwanjani pale aliondoka na taxi hadi hotelini. Timu yetu ilimfuatilia na kumuona mara alipofika hotelini akakutana na Pamela David Kirrita aliyekuwa aupokee huo mzigo”, alisema Mkurugenzi wa NCB tawi la New Delhi.

 Amesema walipohojiwa Kirrita aibainisha kuwa alikuwa akiishi katika hoteli moja katika kitongoji kiitwacho Vasant Kunj tokea Januari, na kwamba alikuwa na mawasiliano na mtu mwingine raia wa kigeni ambaye ndiye angempasia mzigo baada ya kuuchukua toka kwa Mkandawire.

Polisi wanasema mzigo ulifichwa kwenye uwazi wa begi la safari, na kwamba Mkabdawire aliwaki kukamatwa nchini Pakistani mwaka 2015 na kukaa mahabusu kwa zaidi ya miezi sita, huku Pamela akikiri kutembelea  India zaidi ya mara sita tokea mwaka 2006.

Kwa sheria za India, mshtakiwa atayekutwa na hatia ya madawa ya kulevya yaliyokuwa ya kibiashara ni kifungo cha kati ya miaka 10 ama 20 gerezani na faini ya Rs 1 lakh (sawa na dola za Kimarekani 15,000) ama Rs 2 lakhs (dola 3000).


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...