Thursday, March 2, 2017

Ajali hii imetokea muda huu hapa External jijini Dar


Chanzo inadaiwa kuwa ni uzembe wa Polisi wa usalama barabarani. Askari amemsimamisha Dereva wa Roli mita 10 kutoka taa za barabarani..huku mwenye boda akiwa nyuma ya Roli ...
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa mwenye Boda alipojaribu kukwepa Roli hilo akagongwa na Roli lingine nakufia hapo hapo...fuvu la kichwa likapasukia ndani ya Element yake.
Baada ya tukio wananchi wakagoma kutoa ushirikiano kwa Askari umati mkubwa uliokuwa eneo hilo wakigomea magari binafsi kubeba mwili wa marehemu....
Hata gari la polisi ilipofika eneo la tukio kwa ajili ya kubeba mwili bado wananchi wakagoma kubeba mwili kwa madai kuwa ni uzembe wao. Mbaya zaidi Askari aliyesababisha ajali hiyo akikimbilia kituoni kwa aibu na woga wa kupigwa na wanachi.



No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...