Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa wasanii na watu wenye majina makubwa ndio wanaoonekana zaidi katika athari za madawa ya kulevya ingawa wapo wengi katika jamii wanayotumia madawa hayo.
Nape Nnauye ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Bunge, Mjini Dodoma alipokuwa akitoa majibu kwa waandishi wa habari waliotaka kujua namna ambavyo wizara yake imelipokea sakata la kukamatwa kwa wasanii ambao wanatuhumiwa kutumia madawa ya kulevya.
“Kama wizara inayosughulikia suala la wasanii tunaunga mkono juhudi zozote za kupambana na jambo hili kwa sababu mwisho wa siku sehemu ya wadau wetu wanaathirika, hivyo basi juhudi za kupambana nalo zinaokoa wadau wetu,” alifafanua Nape Nnauye.
Aliendelea kwa kusema kuwa kama wizara inayosimamia wasanii wamekuwa wakijadili na kuzungumza juu ya athari hizo za madawa ya kulevya kwa wasanii, aidha wapo wasanii ambao Serikali imewasaidiwa kupata matibabu kutokana na athari za madawa hayo, akiwemo mwanamuziki Rehema Chalamila anayefahamika kama Ray C.
Aidha amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo hivyo hawajibiki kuuliza Wizara hiyo anapotaka kuchukua hatua zozote kwa wasanii waliopo ndani ya mkoa anaosimamia, lakini anapohitaji anaweza kuiuliza wizara hiyo.
Nape Nnauye amesema kuwa ni kazi kubwa sana kwa mtu kutengeneza jina (brand) lakini ni rahisi sana kubomoa, hivyo basi ni vyema busara ikatumika katika kuwashughulikia waathirika, vile vile watu wasihukumiwe kwa tuhuma.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitangaza majina ya watu wanaotuhumiwa kuuza ama kutumia madawa ya kulevya wakiwemo wasanii, maaskari na wafanyabiashara na kuwataka kuripoti Polisi kwa ajili ya mahojiano.
Sunday, February 5, 2017
makubwa ndio wanaonekana zaidi katika athari za madawa ya kulevya – nape nnauye.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New Posts
IJUE SCANIA P380[Mende]
Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...
-
Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...
-
Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, ida...
-
Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wameshiriki mkutano wa mwaka 2023 wa mtandao wa polisi wanawake duniani (IAWP) nchini New Zealand. Mk...
No comments:
Post a Comment