Mhe. Temba ambaye ni msanii na kiongozi wa kundi la Yamoto Band amefunguka na kuweka wazi mipango ya kundi hilo na kusema wapo tayari kuachia kazi mbili za Yamoto Band ndani ya siku mbili zijazo.
Akizungumza na eNEWZ Mh Temba amesema alikuwa na mpango wa kuachia kazi yake lakini inabidi asubiri kwanza Yamoto Band watoe kazi zao kwani ni muda mrefu sasa hawajaachia kazi na wananchi wanawasubiri.
"Kwa mwezi huu kuachia kazi yangu itakuwa uongo, mwezi huu tunatoa kazi ya Yamoto Band tuna 'two days remaining' tutaachia kazi ya Yamoto Band ambazo ni nyimbo mbili itabidi tuzipe kwanza nafasi nyimbo zao kwanza ziende miezi kama miwili hivi ndiyo nitakuja kutoa mimi. Yamoto Band wamekaa sana saizi ni kama wana miezi sita hawajatoa kazi mpya hivyo mahitaji ya mashabiki ni kuwasikia Yamoto Band". Mh Temba alisema
No comments:
Post a Comment