Mkurugenzi wa vitengo vya ujasusi nchini Marekani James Clapper amesema kwamba Marekani haijapata changamoto kubwa ya kuingiliwa uchaguzi wake zaidi ya vitendo vya Urusi katika uchaguzi huo wa urais.
Bwana Clapper alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa uchunguzi wa maseneta wa Marekani kuhusu uhalifu wa mtandaoni kabla ya uchaguzi huo.
Ameonya kuwa uhalifu wa mtandaoni unaotekelezwa na Urusi ni tishio kubwa kwa serikali ya Marekani ,lakini udukuzi wa Urusi haukubadilisha jumla ya kura.
Rais mtule Donald Trump alikuwa ametilia shaka hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi huo, lakini katika ujumbe wake wa Twitter siku ya Alhamisi alisisitiza kuwa mfuasi mkubwa wa vitengo vya ujasusi nchini Marekani.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za ulinzi, John McCain alisema kuwa lengo la uchunguzi huo halikuwa kutilia shaka matokeo ya uchaguzi.
No comments:
Post a Comment