Baadhi ya Mabehewa ya TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.
Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa leo Januari 29, 2017 mnamo saa 9:40 alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali . Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia.
Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.
Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika!
Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa .Mkuu wa TRL Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi , Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S. Chillery wako katika eneo la ajali! .
Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es Salaam na inatarajiwa kuwasili saa 2 usku.
Aidha uongozi wa TRL umehakikisha umma na wateja wake kuwa njia ya reli kati ya Ruvu na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji zirejee kama kama kawaida.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 29, 2017
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment