Mwanamuziki Ben Pol amefunguka na kuweka wazi ukweli kuhusu tuhuma za yeye kuiba Idea ya wimbo wa 'Phone' ambao amefanya na Mr Eazi
Ben Pol amesema katika wimbo wake wa 'Phone' Verse ameandika yeye neno kwa neno na sehemu ambayo ameimba Mr Eazi ameandika Eazi mwenyewe na kusema katika wimbo huo Producer Tiddy Hotter alimpa Idea ile ya 'Baby oohh why you check my phone' ambayo ndiyo Sappy amekuwa akisema ya kwake.
"Unajua saizi mimi nafanya kazi na Tiddy Hotter siku moja akaniambia Ben Pol kuna beat moja nataka kukupa sijui na wewe utaipotezea kama wengine? Nikamwambia nipe na wakati ananipa ile beat tayari yeye alikuwa amefanya chorus hivyo mimi nikaandika verse mbili na kufanya baadaye alivyokuja Mr Eazi niliitoa verse moja na kuongezea jambo kwenye chorus ile" alisema Ben Pol
Ben Pol anadai producer Tiddy Hotter alimsisitiza sana kuhusu kazi hiyo na kumtaka ifanyie kazi siyo kama wengine ambao amekuwa akiwapa idea harafu wanashindwa kuzifanyia kazi idea hizo.
"Kiukweli Tiddy Hotter alipokuwa ananipa hiyo beat alisisitiza sana kuifanyia kazi na nikaifanyia kazi ila nachoweza kusema Sappy namwambia afanye kazi aache mambo ya kiki hayawezi kumsaidia maana huyo Sappy nilishawahi kufanya naye kazi nikiwa na Nameless lakini akaivujisha kazi yangu, hivyo aache ujanja ujanja apige kazi mbona wenzake kina Nahreel, Mensen Selekta wanapiga kazi na kazi zao zinasikika aache maisha ya kiki. Kwangu mimi hili alilofanya halijaniathiri kabisaa kwanza ndiyo nimeongeza downloads kwangu kwa hiyo mtu anaye loose ni yeye" alisema Ben Pol
No comments:
Post a Comment