Sio Tanzania pekee wimbo wa Lameck Ditto ‘Moyo Sukuma Damu’ ndio unafanya vizuri, hata nje ya mipaka wimbo huo ni kiboko yao.
Muimbaji mkongwe wa Kenya, Nyota Ndogo amethibitisha ukali wa wimbo huo na akiwaambia wakenya wakubali kuwa muziki wa Bongo Fleva ni moto kwa sasa. Kupitia mtandao wa Instagram, Nyota Ndogo ameweka kipande cha video akiimba wimbo huo na kuandika, “MOYO SUKUMA DAMU SAVINGINE GAI WATANZANIA WAMETUSHINDA NA LYRICS HIO TUKUBALI TUKATAE NDIO UKWELI ULIOPO.”
Hizi ni baadhi ya chati za kwenye mtandao huo za Nyota Ndogo na msanii wa filamu wa Tanzania, Esha buheti wakiuzungumzia wimbo huo.
No comments:
Post a Comment