Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (anayeshughulikia Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameteua wajumbe wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Dhamana ya Hifadhi ya Mazingira Nchini (National Environmental Trust Fund - NETFUND).
Waziri huyo amefanya uteuzi huo leo jijini Dar es salaam kufuatia uamuzi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumteua Ali Mafuruki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko huo.
Mh. Waziri Makamba amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Sheria ya mazingira Sura ya 191 ya mwaka 2004, kifungu cha 215 (2).
Uteuzi huo ni kufuatia mabadiliko madogo yaliyofanyika hivi karibuni kwenye Sheria ya mazingira ambapo Bodi itakuwa na uwezo na mamlaka ya kualika mtu yeyote ambaye siyo mjumbe kushiriki katika maamuzi pale inapoona inafaa
Amewataja wajumbe walioteuliwa kuwa ni Mwajuma Mbogoyo, Emelda Teikwa, Profesa Razak Bakari Lokina na Hatibu Senkoro.Wengine ni Alesia Mbuya, Baraka Juma Kalangahe,Dkt. Andrew Komba na Profesa Yunus Mgaya.
Mhe. Makamba amesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja na kuwatakia kila la heri wajumbe wapya wa Bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yao kama yalivyoainishwa katika Sheria.
No comments:
Post a Comment