Msanii wa filamu nchini, Haji Adam a.k.a Baba Haji amekiri rushwa ya ngono kukithiri katika tasnia ya filamu nchini huku akiweka wazi kuwa kwa upande wake hajawahi kuomba wala kukubali rushwa hiyo kwa hofu ya maradhi.
Baba Haji aliyekuwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV kinachoruka kila Ijumaa saa 3:00, amesema mabinti wengi wenye ndoto za kuigiza, hutumia mbinu mbalimbali ili kupata nafasi za kuigiza kwenye movie za wasanii wakubwa, na mbinu mojawapo ni kuwa tayari kutoa rushwa hiyo kwa wahusika ili kupata nafasi.
"Ni kweli rushwa ya ngono ipo na mimi nilishaingia kwenye mtego, kuna binti mmoja alitaka kunihonga, lakini sikuwa tayari maana kuna maradhi mengi, naogopa maradhi"
Katika hatua nyingine, Haji amesema kuwa yeye ndiye aliyemtoa Aunt Ezekiel bila rushwa ya aina yoyote na kuwataka mabinti wenye vipaji kutegemea uwezo wao kutoka badala ya kutoa rushwa ya ngono, "Mimi ndiye niliyemtoa Aunty Ezekiel, baada ya kumuona nikagundua kuwa anaweza kuwa msanii mzuri, wakati huo mwaka 2001 tulikiwa Ilala, tunaishi kwenye getho, lakini kilichombeba ni uwezo wake na siyo rushwa" Amesema.
Kuhusu mwenendo wa tasnia ya Bongo Movie, ameonesha kupingana na wanaodai kuwa Bongo Movie inaporomoka, na kusisitiza kuwa kwa sasa tasnia ya filamu nchini inakua na wasanii wanapata mafanikio.
Pia alitumia nafasi hiyo kukanusha tetesi za kuoa mke mwingine akisema kuwa mke ni mmoja tu na ndiye aliyefunga naye ndoa, lakini waliachana baada ya mwaka mmoja wa ndoa na kwa sasa hawako pamoja tena, isipokuwa anahudumia mtoto waliozaa pamoja. Amesema kwa sasa yuko 'single' lakini ana watoto wawili
No comments:
Post a Comment