Monday, January 9, 2017

‘Pacha’ wa Harmonize aangua kilio stejini




 HARMO Rapa ambaye ni ‘pacha’ wa msanii wa Bongo Fleva anayebamba na ngoma kibao ikiwemo Matatizo na Bado, Harmonize amejikuta akiangua kilio stejini baada ya kukutana kwa mara nyingine tangu kupita muda mrefu.

Tukio hilo ‘ameizing’ lilijiri juzikati kwenye Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama jijini Dar ambapo Harmonize aliongozana na Dully Sykes na Queen Darleen katika kupiga shoo ya kuufungua mwaka mpya.

Kwa kile ambacho Harmonize hakukitegemea, mapema wakati anaingia ukumbini hapo, Harmo Rapa alikuwa ametega getini kwa shauku ya kumuona ambapo alipofi ka alitumia kila njia ya kuongea naye bila mafanikio kutokana na kuzuiliwa na mabaunsa.

Wakati shoo ikielekea ukingoni ndani ya ukumbi huo ambapo Harmonize alikuwa stejini, Harmo Rapa akaona isiwe ‘kesi’ akavamia jukwaa na kumkumbatia pacha wake huyo huku machozi yakimtoka jambo lililoamsha shangwe ukumbini hapo.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...