Friday, January 6, 2017

Helmeti zatajwa kuwa chanzo cha maradhi ya ngozi

Dodoma. Wakati Sheria ya Usalama Barabarani inamtaka kila dereva wa bodaboda kuwa na kofia ngumu (helmeti) mbili kwa ajili yake na abiria, watumiaji wa vyombo hivyo wapo hatarini kuambukizwa maradhi ya ngozi.

Hatari hiyo inatokana na matumizi ya helmeti chafu.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk James Kiologwe alisema watumiaji wa usafiri huo wamekuwa wakitumia helmeti moja bila kujali kama imefanyiwa usafi, huku wengine wakilazimika kuvaa zilizo chafu ili kutekeleza matakwa ya sheria.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...