Friday, January 6, 2017

Mrundi jela miaka 2 kuingia nchini kinyemela


Raia huyo kutoka Myinga nchini Burundi aliyefahamika kwa jina la Aisha Kwezilamana (26), alifikishwa mahakamani hapo baada ya kukamatwa Desemba 29, 2016, alasiri eneo la Bijampola mjini Kahama.

Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu wa mahakama hiyo, Imani Batenzi, alisema mshtakiwa alipatikana na hatia ya kuingia na kuishi
nchini kinyume cha sheria, hivyo kumpa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka miwili jela kulipa faini ya Sh. 500,000.

Mwendesha Mashtaka wa Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Kahama, Salum Salum, aliiambia mahakama hiyo kuwa mshtakiwa Kwezilamana, aliingia nchini kinyume cha sheria za nchi na kukamatwa eneo la Bijampola Desemba 29,2016 majira ya alasiri.

Mwendesha mashtaka huyo alidai kuwa kuingia bila kibali, alivunja sheria za nchi.

Mshtakiwa huyo alikiri kosa hilo, hivyo mahakama kumtia hatiani kwa kumpa adhabu hiyo ambayo alianza kuitumikia mara moja.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...