Huwenda ukakutana barabarani na Hanifa Daud ‘Jennifer’ pamoja na Othman Njaidi ‘Patrick’ ambayo ni zao la marehemu Steven Kanumba na usiwafahamu kwa jinsi walivyokuwa wakubwa.
Vijana hao wawili walifanya vizuri ndani ya filamu ya Uncle JJ pamoja na This Is It wakiwa na marehemu Steven Kanumba.
Jennifer ambaye mwaka 2014 alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu aka Nisha, amehitimu kidato cha nne mwaka huu.
Kwa upande wa Patrick 2016 alihojiwa na mtandao mmoja wa habari nakudai hana mazuka wa kuigiza kwa sasa kama zamani. Angalia picha zao hapa.
No comments:
Post a Comment