David Burhan enzi za uhai wake.
Dar es Salaam. Kipa wa Kagera Sugar David Burhan amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Akizungumza na gazeti hili asubuhi hii, Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein amethibitisha taarifa za kifo cha mchezaji huyo na kusema klabu imeondokewa na mchezaji wake muhimu.
“Ndio,Burhan amefariki saa 12 asubuhi ya kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu…ni huzuni lakini tunamwachia Mungu,” amesema Hussein na kuahidi kutoa taarifa zaidi baadaye kuhusu kifo cha mchezaji huyo.
Enzi za uhai wake mchezaji huyo pia aliwahi kuichezea Majimaji ya Songea na Mbeya City ya Mbeya.
No comments:
Post a Comment