Thursday, January 5, 2017

Wolper Kumwaga Harmonize ni kiki?

NGULI wa sanaa ya maigizo wa Bongo ajulikanaye kama Jeniffer Lopez wa Bongo,  mrembo Jacqueline Wolper ‘Gambe’ na msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo kubwa ya muziki Bongo, Harmonize, penzi lao lineaendelea kudhihirika wazi kuwa ni penzi la maigizo.

Wawili hao licha ya kuwa penzi lao lilikosa kuaminiwa na wengi tokea awali, waliendelea kuonyesha wazi kuwa wameshibana na wameamua kuwa pamoja. Mwaka jana katika mitandao ya kijamii ziliwekwa picha na wawili hao wakiwa sehemu mbalimbali kama vile katika shoo kadhaa huko Mtwara, mbuga za wanyama na sehemu zenye kulipa uhai pendo.

Januari 5 mwaka huu wawili hao wameianza siku katika hali ya utata ikiwemo kufuta picha za pamoja katika mitandao ya kijamii na Wolper kuandika maneno haya instagram:
“Nina akili timamu me syo mtoto endelea na maisha yako It is over sasa waambie rasmi usifiche tena @harmonise_tz I hate love”.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...