Monday, January 30, 2017

TFF yaguswa na Kifo cha mchezaji wa Kagera Sugar

 Shirikisho la Kandanda nchini Tanzania TFF limesema kuwa limepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Burhan mchezaji wa Kagera Sugar ambaye mefariki usiku wa kuamkia leo.

Kupitia ukurasa wake wa twitter rais wa shirikisho ls soka Jamal Malizi aliandika haya "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar.Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani.alisema Malizi.

Mapema hibvi leo taarifa za msiba wa Kipa wa Kagera Sugar, David Burhani zilianza kuvuma haswa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba amefariki dunia.

David Buruhan kipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki katika Hospital ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa baada ya kusumbuliwa na Malaria, Burhani aliwahi kuichezea Mbeya City na baadaye aliweza kujiunga na Majimaji ya Songea na kuitumikia msimu mmoja.

Taarifa zaidi endelea kufuatilia taarifa zetu.




No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...