Thursday, January 5, 2017

“Nathibitisha rasmi, ndio… niko Single” – Nicki Minaj

 Baada ya kuwepo tetesi mitandaoni kuhusu staa wa Hip Hop, Nicki Minaj kutoka YMCMB Marekani, zikidai kuwa ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu rapa Meek Mill kutoka Philadelphia na member wa crew ya MMG, finally imethibitishwa rasmi na Nicki Minaj mwenyewe kwamba yuko single.

Female rapa na mmiliki wa Brand ya Pink Print amethibitisha leo January 5, 2017 saa 11:16 jioni kupitia Twitter Account yake kwamba hayuko tena kwenye uhusiano na anachokiangalia kwa sasa ni kazi yake kama msanii na ataanza kuziachia kazi zake siku chache zijazo.

Ripoti za kuachana kwa Nicki na Meek zilianza kusambaa December 2016 wakati Meek Mill alipoamua kuifuta account yake ya Instagram na baada ya muda Nicki akapost kitu kuonesha wawili hao hawako poa tena. Japokuwa hakuna aliyezungumza chochote kuhusu kuachana kwao, Meek alipost picha ikionesha akiwa na mwanamke kitandani na hakuwa Nicki.

Kumbuka mapenzi ya Nicki na Meek yanavunjika ikiwa ni miaka miwili tu tangu waanza kuwa wapenzi baada ya Nicki kuachana na aliyekuwa mpenzi wake wakati huo, Safaree.


No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...