Thursday, January 5, 2017

Ajinyonga kwa kunyimwa na mkewe samaki mbichi

MKAZI mmoja wa kijiji cha Kalundi kilichopo kata ya Kipande wilayani Nkasi, Vedast Kazumba (51) amejiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa alighadhabika, baada ya mkewe kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alithibitisha tukio hilo.

Alisema ni la usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya na kwamba Kazumba alifikia uamuzi huo mgumu kwa kujinyonga akitumia kamba ya katani .

Alieleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na polisi kuhusu tukio hilo na uchunguzi wake unaendelea . Habari kutoka kijijini humo, zinaeleza kuwa chanzo cha Kazumba kujinyonga ni kukasirishwa na kitendo cha mkewe, Antoniata Mwisua kumnyima kitoweo cha samaki mbichi.

“Mke wa marehemu aitwae Antoniata alimwandalia mumewe huyo chakula cha usiku, kitoweo chake kikiwa ni samaki mbichi alimkomba samaki huyo kisha akamwomba amwongezee kitoweo kingine cha samaki, lakini mkewe alimweleza kuwa kitoweo hicho kimekwisha. Ndipo mumewe alipokasirika akidai kuwa mkewe amemnyika kwa makusudi kitoweo hicho ndipo alipochukua hatua ya kuzira kula“ alieleza mmoja wa mashuhuda kwa masharti ya kutoandikwa gazetini.

Akizungumzia mkasa huo , Mwenyekiti wa Kijiji cha Kalundi , John Kalasa alidai kuwa marehemu wakati wa uhai wake alikuwa ni mtu mwenye kujawa na ghadhabu ambapo mara kadhaa alisikika akitishia kujinyonga.

No comments:

Post a Comment

New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...