Sunday, January 29, 2017

Newz Alert: Treni Ya Deluxe Iliyopata Ajali,Hakuna Vifo Vilivyoripotiwa

 Baadhi ya Mabehewa ya  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

 Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetoa taarifa kuwa leo  Januari 29, 2017 mnamo  saa 9:40 alasiri treni ya abiria ya Deluxe ilipokuwa ikirejea Dar es Salaam kutoka Kigoma imepata ajali kati ya vituo vya Ruvu na Ngeta ambapo mabehewa 9 yamepata ajali . Kati ya hayo manne yameanguka, mawili yametenguka na matatu yameacha njia.

Imeripotiwa watu kadhaa wamepata majeraha mepesi isipokuwa mmoja ndiye aliyepata majeraha makubwa ambaye amekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Hizi ni taarifa za awali baada ya Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndio taarifa ya kamili ya ajali itakamilika!

Wakati taarifa hii ikipatikana Waziri wa  Ujenzi na Uchukuzi  Profesa Makame  Mbarawa  .Mkuu wa TRL Ndugu Kagosa Kamanda Kikosi , Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Nd Masanja Kungu Kadogosa na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Reli Mhandisi S. Chillery wako  katika eneo la ajali! .

Halikadhalika taarifa imefafanua kuwa sehemu ya treni ya Deluxe yenye mabehewa kumi na abiria wake iko njiani kuja Dar es Salaam na  inatarajiwa kuwasili saa 2 usku.

Aidha  uongozi wa TRL umehakikisha umma na wateja wake kuwa njia ya reli  kati ya Ruvu na Dar es Salaam itafunguliwa ndani ya saa 24 ili shughuli za usafirishaji  zirejee kama kama kawaida.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
 Kwa niaba ya  Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Masanja Kungu Kadogosa
Januari 29, 2017
DAR ES SALAAM

No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...