Monday, January 9, 2017

Ma Dj Wa Sauzi Waufagilia Muziki Wa Bongo

Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ (kushoto) na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ (kulia) wakizungumza na Waandishi wa Habari jana

WACHEZESHA disko ‘ma DJ’ maarufu Afrika Kusini Siyabonga Sibeko ‘DJ Capital’ na Lutendo Kungoane ‘Dj Sliqe’ wamesema kwamba muziki wa Tanzania uko juu kwa sasa.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari jana katika hoteli ya New Africa, Dar es Salaam ma DJ hao wa Redio na Telesheni nchini Afrika Kusini walisema Tanzania imepiga hatua kubwa kimuziki.

“Kwa sasa huwezi kuzungumzia nchi zinazofanya vizuri kwa kiwango cha juu kimuziki Afrika bila kuitaja

Tanzanja,”alisema Dj Capital na kuongeza; “Afrika Kusini, Nigeria, Ghana, Tanzania na Kenya hizo ndizo nchi za Afrika zinazofanya vizuri katika muziki wa kisasa,”alisema.

Kwa upande wake DJ Sliqe’ alisema kwamba anavutiwa zaidi na wasanii wawili wa Tanzania kwa sasa, ambao ni Diamond Platnumz na Vanessa Mdee.

“Ni wasanii wengi wa Tanzania wanaofanya vizuri kwa sasa, lakini mimi upande wangu nawapenda zaidi hao wawili,”alisema.

Wawili hao, wote ni Ma DJ wa kituo cha Redio cha Touch Central cha Johannesburg, Afrika Kusini wakati DJ Capital pia anafanya kipindi cha Club 808 cha Televisheni ya ETV nchini humo.

Wawili ambao wamekuja nchini kwa ziara ya wiki moja kujifunza zaidi kuhusu muziki wa Tanzania, pia ni Ma DJ wa kumbi za disko nchin kwao.

“Tumekuja hapa kujigunza na kukutana na wasnaii kwa sababu sisi pia ni watayarishaji wa muziki,”alisema Capital.

No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...