Sunday, January 29, 2017

Breaking Newzz: Mabehewa Matano Ya Treni Ya Mwendo Wa Haraka (Deruxe) Yaanguka Pwani Ikitokea Kigomo Kuja Dar

 Baadhi ya Mabehewa ya  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, yakiwa yameanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

  Baadhi ya Mabewa mengine yakionekana kuacha njia


Baadhi ya Abiria waliokuwa wamependa  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam,wakitoka kwenye mabehewa hayo mara baada ya kupata ajali eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

  TRENI ya mwendo haraka, (DELUX), iliyokuwa ikitokea Kigoma kuja jijini Dar es Salaam, imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani jioni hii ya Januari 29, 2017.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka eneo la ajali,zinaeleza kuwa takriban mabehewa 10 yameanguka na juhudi za kuwaokoa watu zilikuwa zikiendelea,aidha imeelezwa kuwa watu kadhaa walionekana wakiwa wamelala chini wengine hawajiwezi kabisa.

Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, na alipoongea na mwandishi wa habari hizi majira ya saa 11;13 jioni, amesema treni hiyo imeanguka na ni mabehewa matano ya abiria yameanguka na moja limeacha njia, lakini hakuwa na taarifa zaidi kwani ndio alikuwa anajiandaa kuelekea eneo la tukio.

“Ni kweli treni yetu ya Delux iliyokuwa ikitokea Kigoma na kutarajiwa kuwasili hapa saa 11:30, imeanguka eneo la Ruvu, na mabehewa matano yameanguka na moja limeacha njia, taarifa zaidi tutazitoa kuhusu walioathirika kwa sasa tunajiandaa kwenda eneo la tukio” Alisema Maez.

Taarifa zaidi zitawajia kadri zitakavyotufikia.

No comments:

Post a Comment

New Posts

Libya yatangaza hali ya dharura ya mwaka mzima baada ya mafuriko

  Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...