Msanii Christian Bella amefunguka na kusema kuwa mara nyingi hata 'idea' ya muziki wake zinatoka kwa msanii Chris Brown kutoka Marekani na kusema ni kati ya wasanii ambao anasikiliza sana kazi zao.
Christian Bella akiongea na EATV amedai kuwa anapenda kumsikiliza sana kazi za Chris Brown kwanza ni kutokana na ukweli kwamba anampenda msanii huyo lakini pia kingine ni kutokana na majina yao kufanana.
"Mimi kusema kweli sina 'Role model' bali mimi napenda muziki mzuri lakini kwa kizazi chetu ukiangalia kwa nje nampenda sana Chris Brown na nasikiliza sana kazi zake, kwa sababu kwanza tunaendana majina ( CB ) Christian Bella, Chris Brown, yaani na mimi ni Breezy vile vile, yaani jamaa ana flow flani ambazo mimi mwenyewe nikimsikiliza nasikia raha lakini hata njia zake pia na feeling zake naposikiliza huwa zinanipa idea, zinanisaidia idea za kuimba lakini huwezi kuelewa kwamba kuna flow flani kwenye kazi zangu kupitia kumsikiliza Chris Brown ndiyo niliweza kuzipata" alisema Christian Bella
Mbali na hapo Christian Bella amesema kwa wasanii wa bendi, msanii anayemkubali na kusikiliza sana kazi zake ni Koffi Olomide, kwani anadai msanii huyo amefanya mambo makubwa sana kwenye muziki wa dansi nchini DRC
Wednesday, March 1, 2017
Mwanamuziki Christian Bella anachota idea kwa msanii huyu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
New Posts
IJUE SCANIA P380[Mende]
Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...
-
Serikali ya Libya imetangaza hali ya dharura ya mwaka mzima kwa shabaha ya kuzuia kuenea magonjwa ya kuambukiza katika maeneo yaliyokuumbw...
-
Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema leo Jumatatu kuwa imenasa ndege 103 za kivita za China karibu na kisiwa hicho katika muda wa saa 24, ida...
-
Askari wa kike kutoka nchini Tanzania wameshiriki mkutano wa mwaka 2023 wa mtandao wa polisi wanawake duniani (IAWP) nchini New Zealand. Mk...
No comments:
Post a Comment