Friday, April 14, 2017

Obby Claud Blog Tunakutakia Heri ya PASAKA


Bwana Yesu Asifiwe!
Tunamshukuru Mungu Baba kwa kutupa neema hii ya kushirikishana Neno la Mungu kwa Njia hii tena. Kesho tutakuwa tukiadhimisha sikukuu ya Pasaka, na makanisa mengi hivi sasa yapo kwenye majira ya kiibada ya Pasaka. Na Mungu ashukuriwe kwa kutupa neema ya kuadhimisha Pasaka katika mwaka huu wa 2012.
Wewe kama mwana wa Mungu, hupaswi tuu kuadhimisha Pasaka kwa mazoea, bali inakupasa na ni vyema sana kuadhimisha Pasaka kuanzia moyoni mwako, kwani Mungu anawatafuta watu watakaomwabudu katika roho na kweli.( Yohana 4:23 ), hivyo basi, napenda kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tuyatafakari mambo machache kuhusu siku kuu hii ya Pasaka.
HISTORIA YA PASAKA
Katika Biblia, Pasaka ilianza kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Kutoka 12, tafadhali tenga muda ukisome kitabu hiki kizima. Katika Pasaka hii ya kwanza, wana wa Israel waliagizwa kupakaa damu ya kondoo kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango yao kabla ya Mungu kuleta pigo la kumi kwa watu wa Misri, ambalo lilikuwa ni pigo la kuwauwa wazaliwa wote wa kwanza wa Wamisri.
Mungu aliagiza WaIsrael wapakae damu hiyo kwenye milango yao ili Malaika atakapokuwa anapita kuwaua wamisri, asiwaue na WaIsraeli pia. Na Malaika alipokuwa akipita, aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Wamisri, na aliacha kudhuru kila nyumba ya WaIsraeli, mradi tuu iwe imepakwa damu ya kondoo mlangoni.


DAWA ILIKUWA YA LAZIMA
Katika Kutoka 12:23, inasema “ BWANA apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu kwenye vizingiti na kwenye miimo ya milango naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zetu na kuwapiga ninyi “. Jambo lililotakiwa hapa ili na Waisraeli wasipigwe, na wao kuweka damu kwenye milango yao. Bwana alichokuwa anaangalia si kuona kama nyumba fulani ni ya Muisrael au la, Yeye alikuwa anaangalia kama kuna damu mlangoni au la. Hii ina maana kuwa kama Mwisrael yeyote asingepakaa damu ya kondoo huyo katika mlango wake, angeangamia pamoja na Wamisri. Umeona msisitizo wa damu katika Pasaka hii ya kwanza? Na siku hiyo ndiyo siku ambayo wazaliwa wa kwanza wa Wamisri walikufa, na Waisraeli wote wakatoka utumwani Misri na kuanza safari ya kuelekea katika nchi ya Kaanani waliyoandaliwa na Bwana.
Na baada ya hayo, Mungu aliwaagiza WaIsrael kuiadhimisha siku hii daima na hata akasema “Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’,Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa BWANA, ambaye alipita juu ya nyumba zetu alipowapiga Wamisri“( Kutoka 12:26-27 ). Kwa hiyo kuadhimisha Pasaka ni agizo la Mungu. Na pia Mungu akaendelea kusema “ Kwa sababu BWANA aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri katika usiku huu Waisrael wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu BWANA katika vizazi vijavyo. ” (Kutoka 12:42 ).
Hivyo ndivyo namna Pasaka ilivyoanza kwa agizo la Mungu mwenyewe, na ukisoma katika Kutoka 12, ndivyo ilivyoendelea kuadhimishwa mara nyingi katika kipindi cha Agano la Kale. Kuna wakati wana wa Israel walikaa muda mrefu sana bila kuadhimisha Pasaka, lakini kila mara alipoinuka mtu aliyeisoma sheria ya Mungu, walitubu na kuendelea tena kuadhimisha siku hii ya Pasaka.
Kwa siku ya leo nimeona nikukumbushe namna Pasaka ilivyoanza ili usiwe unaadhimisha Pasaka kwa namna ya mwili tu, bali uadhimishe Pasaka kuanzia moyoni. Na ikitokea umeulizwa na mtu asiyeamini au asiyefahamu, basi uwe tayari kumweleza kwa upole kuhusu Pasaka. Nitakuletea sehemu ya pili ya somo hili ili kujifunza zaidi pia.


Thursday, March 23, 2017

Maneno ya Nape baada ya taarifa ya kutumbuliwa Uwaziri asubuhi hii




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kumteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo… na taarifa kamili ndio hii hapa chini kutoka IKULU.


Aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye ameandika kupitia account yake ya Twitter ‘Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!’



BREAKING: Rais Magufuli atengua Uwaziri wa Nape Nnauye





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kumteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo… na taarifa kamili ndio hii hapa chini kutoka IKULU.



Tuesday, March 21, 2017

Askofu Gwajima kutinga Clouds Media

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gwajima aliandika....

"Taarifa: Kesho 22/03/2017 saa nne kamili asubuh nitakwenda Clouds Media kuwapa pole kwa yaliyotokea"



Tundu Lissu amtumia waraka Rais Magufuli

Tundu lisu amemwandikia waraka huo mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jonh pombe magufuri akiwa kama raisi wa Tanganyika Law Society (TLS).

Usome waraka hapa chini



Monday, March 20, 2017

Tanzania, Rwanda na Burundi Kati ya Nchi Zenye watu wasio na Furaha duniani.

Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani.
Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini.
Uhaba mkubwa wa wafungwa waikumba Uholanzi
Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha
Bia husaidia watu 'kufungua roho'
Watanzania hutafuta nini mtandaoni?
Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Wezi 13 wajinga zaidi duniani
Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147.

Source: BBC



Magufuli asema Makonda chapa kazi



Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi.

Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa vikali.

Akizungumza Jumatatu hii kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa barabara za juu (Flyovers) Ubungo, Dar, Rais Magufuli amesema, “Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Rais amesema Watanzania wanapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

“Tumepoteza direction tumeanza kujadili personalities,” aliongeza.


New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...