1. Kiongozi wa kambi rasmi ya
upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amezungumzia sababu za kukosekana kwa hotuba
yake Bungeni na kusema Wamegomea Kusoma Hotuba Za Kambi Hiyo Kwa Wizara Yoyote
Mpaka Watumishi Wa Ofisi Hiyo Watakaporejeshwa Kazini.
|
Freeman Mbowe |
2. Moja kati ya stori
inayoshika headlines kutoka nchini Libya ni hii kutoka Mahakama ya Tripoli ambayo
imefuta kesi ya mauaji iliyokua ikimkabili Saadi
Gaddafi, mtoto wa tatu wa aliekua rais wa Libya, Muammar Gaddafi.
Saadi Kaddafi amefutiwa mashtaka yote
dhidi yake katika kesi ya mwanamichezo Bachir al-Rayani ambaye alifariki dunia
mwaka 2006 baada ya kupigwa kichwani, Bachir Rayani alifariki dunia baada ya
malumbano katika nyumba inayomilikiwa na Saadi Gaddafi.
3. Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu inatarajia kutoa uamuzi April 23,2018 kuhusu
kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili mrembo Wema Sepetu na wenzake kama
wana kesi ya kujibu au hapana na uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu
Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi
watano wa upande wa mashtaka.
Mbali na Wema washtakiwa
wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kutumia dawa za kulevya ni Angelina
Msigwa na Matrida Seleman Abbas.
|
Wema Sepetu |
4. wasanii wengi kutoka Zanzibar wamekuwa waisahau fadhila na
kusahau walikotoka hasa pale wanapohamishia majukumu yao kikazi Jijini Dar es
Salaam, huyu hapa ni nedy music kutoka Zanzibar hapa anawajibu mashabiki wake
ambao wanasema amekusahau kabisa Zanzibar.
|
Nedy Music |
5. Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewataka Watanzania wawe
wepesi wa kutoa pongezi pale wasanii wa filamu nchini Tanzania wanapofanya
vizuri, na sio kuwabeza na kuwaponda kila siku kwani kitendo hicho
kinawakatisha tamaa waigizaji wetu.
|
Haji Manara |
Via ➡KingsFmRadio 104.3Mhz
➡KingsFmRadioAndroidApp
➡Tunnein 12:00-12:15 pm
www.kingsfm.co.tz