Monday, June 5, 2017

Breaking News: Halim Mdee na Ester Bulaya wapewa adhabu ya kutohudhuria Bungeni mpaka mwakani






Halima Mdee na Esther Bulaya wamehukumiwa kutohudhuria vikao vyote vya bunge linaloendelea mpaka mkutano ujao wa Bunge la Bajeti ya 2018/19.

Hukumu hiyo imeungwa mkono na wabunge wengi waliopitisha azimio hilo.

Mapema leo, Jumatatu Kamati ya Maadili  ilisema Bulaya na Mdee wamemaliza adhabu za kawaida zilizopo kwenye kanuni za bunge.

Hata hivyo, Bunge liliendelea  kujadili makosa ya wabunge hao wa Bunda na Kawe.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika aliliomba Bunge kujadili adhabu inayostahili kulingana na makosa yao.

Kanuni inasema, mbunge anayefanya kosa la kwanza anaweza akazuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 10 na atayakosea kwa mara ya pili anaweza kuzuiwa kuhudhuria vikao visivyozidi 20.


Friday, April 14, 2017

Obby Claud Blog Tunakutakia Heri ya PASAKA


Bwana Yesu Asifiwe!
Tunamshukuru Mungu Baba kwa kutupa neema hii ya kushirikishana Neno la Mungu kwa Njia hii tena. Kesho tutakuwa tukiadhimisha sikukuu ya Pasaka, na makanisa mengi hivi sasa yapo kwenye majira ya kiibada ya Pasaka. Na Mungu ashukuriwe kwa kutupa neema ya kuadhimisha Pasaka katika mwaka huu wa 2012.
Wewe kama mwana wa Mungu, hupaswi tuu kuadhimisha Pasaka kwa mazoea, bali inakupasa na ni vyema sana kuadhimisha Pasaka kuanzia moyoni mwako, kwani Mungu anawatafuta watu watakaomwabudu katika roho na kweli.( Yohana 4:23 ), hivyo basi, napenda kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tuyatafakari mambo machache kuhusu siku kuu hii ya Pasaka.
HISTORIA YA PASAKA
Katika Biblia, Pasaka ilianza kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Kutoka 12, tafadhali tenga muda ukisome kitabu hiki kizima. Katika Pasaka hii ya kwanza, wana wa Israel waliagizwa kupakaa damu ya kondoo kwenye vizingiti vya juu na miimo ya milango yao kabla ya Mungu kuleta pigo la kumi kwa watu wa Misri, ambalo lilikuwa ni pigo la kuwauwa wazaliwa wote wa kwanza wa Wamisri.
Mungu aliagiza WaIsrael wapakae damu hiyo kwenye milango yao ili Malaika atakapokuwa anapita kuwaua wamisri, asiwaue na WaIsraeli pia. Na Malaika alipokuwa akipita, aliwaua wazaliwa wa kwanza wa Wamisri, na aliacha kudhuru kila nyumba ya WaIsraeli, mradi tuu iwe imepakwa damu ya kondoo mlangoni.


DAWA ILIKUWA YA LAZIMA
Katika Kutoka 12:23, inasema “ BWANA apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu kwenye vizingiti na kwenye miimo ya milango naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zetu na kuwapiga ninyi “. Jambo lililotakiwa hapa ili na Waisraeli wasipigwe, na wao kuweka damu kwenye milango yao. Bwana alichokuwa anaangalia si kuona kama nyumba fulani ni ya Muisrael au la, Yeye alikuwa anaangalia kama kuna damu mlangoni au la. Hii ina maana kuwa kama Mwisrael yeyote asingepakaa damu ya kondoo huyo katika mlango wake, angeangamia pamoja na Wamisri. Umeona msisitizo wa damu katika Pasaka hii ya kwanza? Na siku hiyo ndiyo siku ambayo wazaliwa wa kwanza wa Wamisri walikufa, na Waisraeli wote wakatoka utumwani Misri na kuanza safari ya kuelekea katika nchi ya Kaanani waliyoandaliwa na Bwana.
Na baada ya hayo, Mungu aliwaagiza WaIsrael kuiadhimisha siku hii daima na hata akasema “Watoto wenu watakapowauliza, ‘Sikukuu hii ina maana gani kwenu?’,Basi waambieni, ‘Hii ni dhabihu ya Pasaka kwa BWANA, ambaye alipita juu ya nyumba zetu alipowapiga Wamisri“( Kutoka 12:26-27 ). Kwa hiyo kuadhimisha Pasaka ni agizo la Mungu. Na pia Mungu akaendelea kusema “ Kwa sababu BWANA aliutenga usiku ule ili kuwatoa Waisraeli katika nchi ya Misri katika usiku huu Waisrael wote wanapaswa kuadhimisha kwa kukesha ili kumheshimu BWANA katika vizazi vijavyo. ” (Kutoka 12:42 ).
Hivyo ndivyo namna Pasaka ilivyoanza kwa agizo la Mungu mwenyewe, na ukisoma katika Kutoka 12, ndivyo ilivyoendelea kuadhimishwa mara nyingi katika kipindi cha Agano la Kale. Kuna wakati wana wa Israel walikaa muda mrefu sana bila kuadhimisha Pasaka, lakini kila mara alipoinuka mtu aliyeisoma sheria ya Mungu, walitubu na kuendelea tena kuadhimisha siku hii ya Pasaka.
Kwa siku ya leo nimeona nikukumbushe namna Pasaka ilivyoanza ili usiwe unaadhimisha Pasaka kwa namna ya mwili tu, bali uadhimishe Pasaka kuanzia moyoni. Na ikitokea umeulizwa na mtu asiyeamini au asiyefahamu, basi uwe tayari kumweleza kwa upole kuhusu Pasaka. Nitakuletea sehemu ya pili ya somo hili ili kujifunza zaidi pia.


Thursday, March 23, 2017

Maneno ya Nape baada ya taarifa ya kutumbuliwa Uwaziri asubuhi hii




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kumteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo… na taarifa kamili ndio hii hapa chini kutoka IKULU.


Aliyekuwa Waziri wa Habari Nape Nnauye ameandika kupitia account yake ya Twitter ‘Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!’



BREAKING: Rais Magufuli atengua Uwaziri wa Nape Nnauye





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri ambapo sehemu ya mabadiliko hayo ni kumteua Waziri mpya wa Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo… na taarifa kamili ndio hii hapa chini kutoka IKULU.



Tuesday, March 21, 2017

Askofu Gwajima kutinga Clouds Media

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Gwajima aliandika....

"Taarifa: Kesho 22/03/2017 saa nne kamili asubuh nitakwenda Clouds Media kuwapa pole kwa yaliyotokea"



Tundu Lissu amtumia waraka Rais Magufuli

Tundu lisu amemwandikia waraka huo mhe. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jonh pombe magufuri akiwa kama raisi wa Tanganyika Law Society (TLS).

Usome waraka hapa chini



Monday, March 20, 2017

Tanzania, Rwanda na Burundi Kati ya Nchi Zenye watu wasio na Furaha duniani.

Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani.
Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini.
Uhaba mkubwa wa wafungwa waikumba Uholanzi
Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha
Bia husaidia watu 'kufungua roho'
Watanzania hutafuta nini mtandaoni?
Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Wezi 13 wajinga zaidi duniani
Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini. Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147.

Source: BBC



Magufuli asema Makonda chapa kazi



Tofauti na kile ambacho watanzania wengi leo walikuwa wakitarajia kuona Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli akichukua uamuzi mgumu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, mkuu huyo wa nchi amemuelezea Makonda kuchapa kazi.

Makonda anakabiliwa na kashfa lukuki ikiwemo ile ya kudaiwa kughushi vyeti na kwamba jina lake halisi ni Daudi Bashite, kutumia vibaya madaraka yake ikiwemo tukio la juzi la kuvamia studio za Clouds Media Group akiwa na wanajeshi wenye silaha akilamizimisha kurushwa kwa kipindi na zingine. Tukio hilo limelaaniwa vikali.

Akizungumza Jumatatu hii kwenye uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa barabara za juu (Flyovers) Ubungo, Dar, Rais Magufuli amesema, “Mimi ndio najua mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi, ni mimi ninayepanga. Ninajua wamenielewa. Kwahiyo Makonda wewe chapakazi, nasema chapa kazi.”

“Suala la kuandikwa kwenye mitandao sio tija kwangu, hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao kwahiyo nijiuzulu urais? Chapa kazi, hapa kazi tu.”

Rais amesema Watanzania wanapoteza muda mwingi kwa mambo yasiyo ya msingi.

“Tumepoteza direction tumeanza kujadili personalities,” aliongeza.


Nape asema Kitendo Kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa kimenajisi Tasnia ya Habari




Waziri Nape: Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda

Waziri Nape: Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itasomwa wazi

Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru. Mamlaka zitajua cha kufanya

Kusaga: Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!

Reginald Mengi: Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!

Nape Nnauye(Waziri wa Habari): Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

Nape: Natoa pole kwa Clouds Media na kwakuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

Nape Nnauye: Ripoti itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24\

Habari zaidi....

Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi haijapinduliwa.

Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.

Chanzo : Mwananchi


Saturday, March 11, 2017

Simulizi ya SECRET DOCUMENT(nyaraka za siri)



SECRET DOCUMENT(nyaraka za siri)
MTUNZI: BENCHRYS
SEHEMU YA PILI – 2
0758784299 wasap tu,

Tulipoishia>>>>
Baada ya Jastin kuambiwa vile na yeye hakupoteza muda akaangalia kwa njia ile ambapo lilikuja jina la JACKOB CHARLES taa za kichwa chake kilianza kupekua hili jina mara moja akagundua kwamba ni ‘bestman’ wake ambaye alikuwa ni Jakob, mara moja akanyanyua simu na kuweka sikioni ambapo kwa wakati huu sauti iliyosikika ilikuwa ni sauti ya Jakob mwenyewe ikiwa inaongea kwa furaha sana,,,,,,,,,

Songa nayo>>>
Jastin baada ya kusikia sauti ile imani yake ya kwamba yule ni rafiki yake ambae alitegemea awe ni msimamizi wa  harusi yake amempigia,
“daah sawa Bhana Jakob naona umeamua kunifanyia hivyo powa, uko wapi sasa”
“njoo kwenye ile saloon niliyokwambia”

Basi Jastin nae hakutaka kupoteza hat sekunde nyingi sana kwa mara moja akachukua gari lake prado na kuingia kisha akakanyaga moto, kisha akageuza gari lake kuelekea upande wa kutoka nje ya geti, zoezi hilo halikuwa na muda mwingi sana na kwa mara moja akawa tayari yupo nje, baada ya hapo akavaa stereo bluetooth sikioni ili imsaidie kwa mawasiliano kama kutakuwa na mtu ambae ananmpigia wakatia akiwa kwenye gari anaendesha na huo ulikuwa ni utaratibu wake na  baada ya kuvaa palepale akachukua simu yake na kuwasha bluetooth kisha akaunganisha na kile kifaa chake na kuweka simu kando, akafunga mkanda na baada ya hapo akaanza safaria mbapo ilikuwa ikimpeleka jumla kwenye saloon ambayo alikuwa ameambiwa na rafiki yake, Jakob ambaye alimweka kuwa ni msimamizi wa harusi yake ile.
‘ngrrrrrrrrrrn ngrrrrrrn’
Ni simu ya Jastin ilikuwa ikiita kwa wakati huo aliiona lakini alikuwa kwenye mwendo mkali sana na ilikuwa katika barabara kuna magari mengi sana lakini hiyo haikuwa inasababu ya kumfanya asipokee simu ile, bila kuchelewa akakwepesha jicho moja ambalo liliangalia kwenye simu na baada ya kuangalia aliweza kuona jina la  kwenye simu lililokuwa limeseviwa ‘My lover’  baada ya kuona hilo jina moyo wake ulilipukwa na furaha sana kwa kuwa ilikuwa ni simu ya mpenzi wake ambaye siku inayofuata ilikuwa ikitegemewa ifungwe ndoa takatifu. Basi hakupoteza muda akatumia mkono wake mmoja kushika usukani na mwingine akautumia katika kutafuta batani ambayo ilikuwa kwenye bluetooth ya sikion kwake ili apokee simu na hilo swla halikuwa zito sana kwake, hivo kwa sekunde tu akawa tayari ameshaigusa na baada ya hapo akaipokea simu ya Agatha,
“Darling upo wapi mbona, nipo hapa kwako sikuoni”
“nimeenda kwa Jakob mara moja, ila sio muda mwingi narudi hapo au ntakuja mwenyewe”
“hujalelewa tu kulikuwa na jambo muhimu sana la  kukwambia mpenzi ila basi, fanya uwahi kurudi basi”
“usijali mpenzi sasa hivi tu nipo hapo, alafu nadrive ntakutafuta mpenzi love u”
Jastin alifanya kuaga kwa maana mbele yake kulikuwa na traffik ambao mara zote tabia zao alikuwa akizipata sana kwa kutafutiza kosa ata kama gari lako ni salama kabisa ila njaa kwao iliwafanya wafanye mambo kama hayo,
Baada ya simu kakatwa Jastin alikuwa makini na barabara lakini aliweka nia ya kwamba anawahi kurudi kwa maana alikuwa akihitaji kujua ni jambo gani la muhimu ambalo limemfanya Agatha aondoke nyumbani kwao mpaka kuja kwake na hakujua ni kwa namn gani ameondoka mpaka afike huko kwake kwa maana haikuwa ni jambo rahisi sana kuwatoroka wazee wake kwenye mjadala mzito ambao alikuwa nao kwa muda mrefu sana, ila basi kuhus hayo hakutaka kujaji sana yeye alinyoosha mguu wake na kutaka kufika kwa rafiki yake Jakob,
Akiwa ameshawapita tena wale trafiki wa barabarani akatembea kwa hatua kadhaa simu yake ilianza kuita tena ambapo aliona ni jina la Jakob,
“huyu nae hajui kama ni po njiani” alijisemea Jastin na baada ya hapo ya hapo kapokea simu na kutomwachia nafasi ya kuongea yule ambea alikuwa akimpigia kwa wakati ule,
Ni baada ya kubinyeza tu batani ile ya bluetooth yake,
“Jakob niko njiani sasa hivi nafika”
Aliongea na kubonyeza tena ambapo simu ilikatika bila kusikia sauti ya upande wa pili, yeye safari yake alihitaji ikamilike ili akaongee mengi sana na Jakob na sio kwanjia ya simu na hiyo  ndio ambayo ilimpelekea yeye kukata simu yake kwa mara moja bila kumsikiliza Jakob, mwendo wake kwa kuwa ulikuwa ni mkali sana akawa tayari amefika kwenye saloon ambayo ilikuwa  ameambiwa na Jakob na baada ya kufika pale akafika na kutoa simu yake ili apige, lakini kabla ya yeyey kupiga simu yake ikaanza kuita tena, na alipo tazama jina lilkuwa limeseviwa jako2, akili yake ilishapembua akajua yule ni Jakon kwa namba yake mpya baada ya kuona vile kapokea na kuweka simu sikioni ambapo alisikia sauti toka upande wa pili ikisema “ingia tu nipo ndani” mpaka hapo Jastin hakuw ana nafasi yakuuliza mara ya pili kwa maana alishakuwa amepewa ruhusa na kwa maana alikuw ani tayari amemwona hivyo yeye akanyoosha jumla mpaka ndani ambapo alimwona Jakob akiwa amekaa kwenye sehemu maalumu ya kurekebishia nywele ili zikae katika  mwonekano ambao ni mzuri sana kwa kijana au mzee yeyote kulikuwa na dada mmoja ambae alikuwa nyuma yake anamseti nywele huku akiwa anamfanyia scrab safi kabisa, Jakob kwa jinsi alivyokuwa ametulia usingeweza kudhani kama anaondoka na alikuwa kama ametua shida zake zote, lakini baada ya kuhisi kuna mtu ameingia ilimpasa kushituka kidogo kwa maana alijua ni tayari Jastin ameshaingia pale ndani,
“ooh wao Jastin karibuuuu ila umekawia hatari yani”
“aaa wai sijakawia wala nini sema tu haraka zako na hata umenistukiza”
“daaah habari za huko lakini, ivi ninasiku ngapi sijui sijawatembelea”
“daah tatu ila hujanisusa sana ndugu, dada habari yako” aliongea Jastin na kutupa salamu kwa mtu aliyekuwa akimhudumia Jakob kwa wakati ule
“salama tu kakaangu, karibu ukae chini”
“ooh wao asante”
“vipi shem hawa ndio wenye tukio kesho eeh” ilikuwa ni sauti ya yule mhudumu wa huduma ya kuset nywele na mambo mengine ambapo alikuwa akiuliza kwa Jakob,
“yaah ndio shem wetu huyo kesho anafunga pingu za maisha, vipi mbona umeliza hivyo”
“mmh jamani kuuliza kosa kwani?”
“powa basi ushajua ila na wewe mwongo kwani hukuona ata picha zao?”
“aah acha sikujua mimi< shem heshima yako mahala pako  ni hapa usikae tena huko maana wewe inatakiw aupendeze zaidi yani, wifi mzima?”
Aliongea yule dada huku akiwa anageukia kwa Jastin na kumwonesha kiti ambacho kilikuwa ni maalumu kwaajili ya kupunguza na kuset aina nzuri ya mnyoo utakao kuwapowa sana kwa mtu kama Jastin,
Jastin nae hakuwa na kipingamizi akasimama na kukisogelea kiti kile na baada ya hapo akakaa ili nae aanze kufanyiwa kazi nzuri,

Wakati huo Agatha alikuwa nyumbani kwake akiwa badoa  namngoja Jastin lakini baada ya kukaa sana akagundua huyu hawezi kuwahi hata mara moja, mara moja akachukua kibegi chake kidogo ambapo safari yake ilikuwa kuekelea nyumbani, lakin baada ya kufika kwenye eneo jilani na alipoliacha gari lake,akaonahali ya tofauti ambapo kuna magari mengine mawili yalikuwa yamepaki na hakujua ni akina nani ila akajitoa wasiwasi kwa kuchukulia maana ya kwamba nao watakuwa wanamishe zao mitaa ile,
Agatha alikuwa akiendelea kusogea kwa taratibu mpaka kufikia lile gari ambapo alianza kutoa funguo yake kwenye pocho yake ili akifika pale awe na kazi moja ya kuchokonoa tu gari lake  ili aondoke nalo ili awahi nyumbani,
Hatua moja baada ya nyingine alianza kutembea na kuikaribia gari lake, muda mfupi akawa tayari amefika alitoa funguo zake na baada ya hapo akasogelea mlango huku akishika kitasa cha gari, lakini akajikuta akipigwa na kitu kizito na hapohapo alipoteza fahamu palepale.
               *****

“ndio hivo yani inatakiwa uwe kawaida tu tena hiyo kesho  kujiamini ndio mpango mzima, kuna jamaa aliwahi kunambia eti anakunywa ili awe anawaona watu wote ni kama wadogo zake”
“hahahaaa mi na pombe ni maadui wakubwa sana asee na sihitaji kabisa kwa maana naona ni kama haina faida kwangu, we fikiria ninamawazo ya kuwa na shida ya pesa halafu naenda bar ili tu ninywe eti kupoteza mawazo hiyo hela ningetunzwa siingeongezea baadhi ya kiasi ambacho nilikuwa nakihitaji”
“daaah unamawazo fulani Jastin hadi nimeielewa point yako, zamani mi nilikuwa naona tu baba akinywa na kusema eti pombe ni tamu sana ila kuna siku moja nikataka kuthibitisha kwa kuonjwa duuh mbona nilitema mate mi mwenyewe ata kama haikuwa na harufu mbaya, kwa maana nikali hatari ila wao sijui wanapenda ya nini”
“ hiyo kesho  naingia kama nilivyo wala siwezi kunywa watu ni wakawaida wote hawa tena nafahamu kabisa”
“yaah hivyo ndio inatakiwa pombe inaweza sababisha kuvunja heshima kwa umati wawatu na kusababisha mambo mengine”
“ni kweli kabisa yani”
Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Jastin na Jakob kule saloon, na Jastin kuhusu habari ya Agatha hakuwa akijua chochote, yeye alikuwa tu na amani zote kwanza aliamini kama Agatha akikaa na kuona yeye anachelewa basi ata simu atampigia kwahiyo hakuna shida yoyote ile, alijifariji na baada ya hapo mambo mengine yaliendelea, huku yule dada akiwa kimya tu kuwatengeneza vizuri kadiri ya kazi yake ilivyokuwa ikimpasa kuifanya kwa mana alikuwa akifahamika sana na alikuwa na jina kubwa sana kwa Njombe na baadhi ya maeneo mengine ambako alikuwa amewahi kupewa nafasi yakumfanyia mtu urembo kwaajili ya maandilizi ya harusi au tafrija yeyote ile na licha kuwa na saloon kubwa hiyo badio alikuwana wanafunzi wake ambao wao walikuwa wakihusika na kupamba kwenye maharusi na kuandaa mahali husika ili pawe ni pakuvutia kushawishi waalikwa wa sherehe yenyewe,
Jastin bado alikuwa ametulia huku stori za hapa na pale zikiwa zinaendelea, na baada ya muda ambao ulikuwa si wa kuwachosha sana kazi ilikuwa tayari imeshaisha kabisa, Jastina alisimama na kujiweka sawa lakini akiwa anafanya vile mara simu yake ikaita alipotazama mpigaji alikuwa ni Ngosha,
“hallow Ngosha”
“uko wapi wewe, shem amekuja hadi ameondoka tayari”
“daah ameshaondoka” aliuliza swali la pili huku akijua kabisa nini ambacho kiliongelewa na kweli alikuwa amechelewa sana,
“ndio ameondoka na Dogo amepiga simu kwamba hatawezakuja ila atatuma zawadi”
“daaaaah tayari Yona ameshaniangusha tayari ila sio mbaya nitampigia simu”
Ngosha na Jastin hawakuongea sana simu ya Jastin ilianza kuita ambapo mpigaji alikuwa ni mama yake mzazi, Jastin aliipokea na kuweka sikioni lakin cha ajabu hakusikia sauti yoyote ikiongea, lakini baada ya muda kidogo akasikia sauti ya kike ikiwa inalia,
“mama, mama, mamaaaaa halow kuna nini”
Jastin alipiga ukunga lakini hakuitikiwa na yeyote,,,,,,,,,,
…………itaendeleaa


Friday, March 10, 2017

Thursday, March 9, 2017

Simulizi ya SECRET DOCUMENT(Nyaraka za siri)


SECRET DOCUMENT(Nyaraka za siri)
MTUNZI: BENCHRYS
SEHEMU YA KWANZA – 01
0758784299 wasap tu,
,,,,,,trailer,,,,,
Katika kanisa moja kulikuwa na marumbano baina ya wachungaji waliokuwa watatu na katika marumbano yao yalipelekea mpaka kushikana na kila mmoja hakutaka kukubali kama mwenzake anaweza kumzidi,
“nimesema usinizoee kama lile dili tulisha limaliza sasa tatizo lako nini?”
“ahaaa sasa ngoja nikuonyeshe boya wewe”
“nani boya, nani boya nakuuliza mpuuzi kweli ivi kwakuwa unawaamini wengi unadhani ndio itakuwa ni njia rahisi sana kwako wewe kunishinda mimi, nielewe mbogo wewe mimi ni zaidi yako tena ngoja”
Baada ya kuongea alisimama na kama nyani na kuruka mateke ambayo yalikuwa dabo na kumtulizia mchungaji mwenzake kwenye kifua na hiyo ilikuwa ni kama amemvizia penyewe kwa maana yule mwenzake palepale aliaguka chini huku akiwa anatoa povu jeupe mdomoni kwake,
Baada ya mwenzake kuona amefanya kitendo kama kile hakutaka kupoteza muda hata kwa sekunde moja, palepale akaondoka na kwenda kwenye stoo ya kuhifadhia nguo za kichungaji kabla ya kuvaa na baada ya hapo akaangalia tambala fulani lilikuwa jeupe na kuja nalo kisha akamvalisha yule mchungaji ambaye alikuwa akitoa povu mdomoni kisha akamchukua na kwenda kumwingiza kwenye sanduku fulani ambalo lilikuwa ni la kioo kizito sana,
----secret document----
Ni katika mkoa mpya wa Njombe wilaya ya Njombe Mji, kata ndogo ya Mjimwema kulikuwa na familia ya watoto wa wanne ambapo kila mtoto alikuwa na kazi yake baada ya kuwa wamesoma na kufanikiwa kwa kiwango ambayo kilikuwa kimewaridhisha wao, familia ilikuwa na watoto wanne ambapo majina yao yalikuwa ni Agatha, Dorice, Yona na mmoja ambaye alikuwa wa mwisho ni happy.
Watoto hao wote walikuwa na hali nzuri sana kiafya kimaisha pamoja na mambo mengine, kila siku kulikuwa na maelewani mazuri sana baina yao hao wanne ambapo familia ilikuwa na wasichana watatu huku kukiwa na mvulana mmoja kama kaka yao kwa heshima tunaita hivo.
Maisha yao yalizidi kusonga huku kila mmoja akiwa anafurahia sana kuishi kwa amani na mwenzake, ambapo mwaka 2009 dada yao ambaye alikuwa ni mkubwa wa wote katika familia alitangaza kuwa anatarajia kumtangaza mmewe mpendwa ambaye alikuwa anampenda kwa moyo wote, haikuwana mfano wa kufananisha na mwanaume yeyote kwa jinsi alivyokuwa akimpa asilimia nyingi sana katika moyo wake, mmewe alikuwa akifahamika kwa Jina la Jastin, ambaye nae alikuwa ni wa kutoka dar,
Matangazo yalitangazwa kila mahali hususani kanisani na mahali pengine marafiki zake wengi sana walialikwa kushiriki kwenye ndoa hiyo takatifu, tarehe zilisogea kwa haraka sana ambapo harusi hiyo ilikuwa ni ya tarehe 20/06/2009 siku ya jumamosi,
Katika kuendelea na utaratibu wa kuandaa ndugu na maandalizi baadhi kila mtu alikuwa na makini sana na jukumu ambalo alikuwa amepangiwa na wakubwa,
Agatha yeye alikuwa na jukumu la kuwapigia ndugu na marafiki zake na baadhi ya maclassmate ambao alikuwa akiwakumbuka kwamba walisoma wote, pindi yupo shuleni,
Siku hiyo ilikuwa ni ijumaa kuikaribisha jumamosi ambapo jumamosi ndio ilikuwa ni siku maalumu ya tukio lenyewe, baadhi ya marafiki na ndugu wa jilani walikuwa tayari kwenye nyumba ya akina Agatha,
Dorice yeye alikuwa na kazi ya kwenda kununua kila kitu ambacho kitakuwa kimesalia na ndio ambaye alijua kila ratiba, safari zake nyingi ilikuwa ni kwenda sokoni na kurudi huku akiwa na simu yake sikioni huku anawapa taarifa baadhi ya mrafiki zake.
Nyumba ya jastin na Agatha ilikuwa nii ndogo sana kutokana na kutokana na wageni ambao walikuwa wamefurika lile eneo kutoka pande nyingi sana ikiwemo marafiki wa Jastin upande wa kiume pamoja na wazazi na ndugu baadhi, walikuwa na furaha sana bado Agatha alikuwa anajifikiria hii siku ya kesho itakuaje. Kwamaana hakuwahi kuolewa au kujumuika kwa ujilani sana kwenye shughuli kama hizo. Muda wote yeye alikuwa akingoja tu wamama ambao walikuwa nje ndio wawe waendeshaji wa kila kitu na kubwa ambacho kilikuwa kikifanya mambo yote kuwa sawa kabisa ni kamati kadhaa ambazo walikuwa wameziweka kwa ajili ya muziki, chalula, mapambo na kadhalika,
Yote ilifanywa kwa kutumia gharama kubwa sana na kuhakikisha mambo yanaenda sawa sawia,
“ok ok powa shogaangu usikawie hiyo jamani siunajua tena, alafu kna simu inaingia naomba ukate basi niipokee”
Alikuwa ni Agatha akiwa anaongea kwenye simu yake na hapo akapokea simu nyingine ambapo nayo haikuchukua muda sana,
Jastin nae muda wote alikuwa hayupo mbali sana, alikuwa amekaa na marafiki zake kadhaa ambapo kulikuwa na ngosha wa mtaa uleule wa mjimwema, jina hili alipewa kwa kutokana na kuwa na uwezo mkubwa sana wa kuimba/ kuchana mistari mingi sana ya msanii wa hip hop hapa Tanzania anafamika kwa jina la Fid Q, na jina lake la A.K.A lilikuwa ni NGOSHA hivo nae alipewa jina hilo na kila mtaa alikuwa akifahamika kwa jina hilo,
“asee hivi Jakob umemwona wapi maana nangoja simu yake na wala hapigi,a sije niyeyusha na kesho hiyo maana daah ninahamu sana na siku hiyo”
Aliongea Jastin ambapo alikuwa n kama akimuuliza ngosha na wenzake,
“we usijali tena ngoja nimpigie kabisa kwa maana huyu mkuu nae kwa kuvuta masaa hajambo kabisa,
“daah kweli fanya hivo”
Aliongea Jastin na kunyanyua simu yake ambapo ilikuwa inaita kwa wakati ule kwa namba ngeni,
“mmh nani nae huyu anataka kuleta gezi hapa”
Aliongea Jastin na baadae akageuza simu kuelekea kwa Ngosha, “oya hii namba unaipata?”
“apana ndugu yangu mpokee sikiliza anaongea nini” ulikuwa ni ushauri kutoka kwa Ngosha kwa wakati ule ambapo na yeye alikuwa akihangaika kutafuta namba ya Jakob ili apige na kujua mahali alipo kwa maana alikuwa ameombwa kuwa kama msimamizi au ‘bestman’ kwa siku hizi lilivyozoeleka hili neno,
Jastin hakutaka kupoteza muda sana akapokea simu na kuiweka sikioni ambapo alitulia kimya na kuanza kusikiliza kwa umakini sana ili kujua ni nani anae piga simu kwa wakati ule,
“tafadhali Jastin mbona huongei”
Ilitoka sauti kwenye upande wa pili wa simu ambapo hayo yote yalikuwa yakisikika kwa Jastin lakini alijalibu kuvuta kumbukumbu huyo ni nani anaeongea lakini hakujua bado kwa maana sauti ilikuwa ni ngeni sana kwake, Jastin bado hakutaka kujibu ikiwa hafahamu kabisa mpigaji wa simu ni nani kwa wakati ule,
“hallo Jastin au nakosea namba!!!”
Bado sauti ya upande wa pili haikukata tamaa kwa kuendelea kuongea na Jastin ili iitikiwe,
Jastin baada ya kuona anakaziwa vile akaamua kuongea na,
“Tafadhali ndugu namba ngeni kwani nani mwenzangu?’
“hahahaaaah kumbe sijakosea. Saaasa nilikuwa na ombi kwako Jastin rafiki yangu najua utakuwa umenisahau lakini hakuna tatizo utanikumbuka endapo tutaonana,” akatulia na kuvuta pumzi kidogo kisha akaendelea, “usije sema naongea mengi sana, kaka Jasi eeh kwasasa upo wapi?”
Swali hili lilifanya Jastin ashitule kidogo kwa maana yeye katika kumbukumbu zake alikuwa akikumbuka sauti ya kila rafiki yake na kama kwa ile ingekuwa ni ngeni basi ilipasa aanze kwa kujitambulisha kwanza kwa maana huondio ulikuwa ni utaratibu wake katika simu zozote ambazo alishazoeana na marafiki zake, kiufupi alibaki katika sinto fahamu hakujua bado afanye nini ili kukumbuka huyu ni nani, na kwa gafla tu alijawa na upole kwa maana alijitahdi kukumbuka lakini bado ikawa ni shida kwa upande wake,
“Jastin unawaza nini wakati siku imebakia moja tu, punguza mawazo nduhu yangu hebu jipe shavu kama mimi Ngosha nikiwa namtukuza babu langu ze doni”
Maneni ya Ngosha yalikuwa ni kama ya kufurahisha lakini ndani yake yalikuwa ni ukweli mtupu kwa maana ni kweli hua anamsifu sana Fid q kwa mistari yake kila awapo kwenye kundi la masela wenzake ambao wanapenda sana mziki wa namna hiyo na baadhi ya maeneo ambayo yanaweza yakawa na battle au mashindao juu ya kuchana,
“usishangae sana Ngosha ile namba ni kama siielewi vile kwa maana nimepokea lakini sijamwelewa na sijui ni nani ila yeye anadai kunifahamu vyema sijui nani huyu”
“hhhaaaaha Jasi eeeh acha hizo namba ya mtandao gani hiyo?”
“hii ni sifuri saba hamsini na nne(0754___) nadhani ni voda hii au siyo”
“basi kazi kwisha angalia kwa kifanya kama unatuma pesa kwa hiyo kwenye M-PESA lakini kwenye salio andika salio ambalo linazidi kwenye kiwango ambacho unacho m-pesa huko kisha itume kwa kuthibisha namba moja, kazi simpo tu wataleta jina lake na utajua tu”
“aah kumbe rahisi namna hiyo, ngoja kwanza”
Baada ya Jastin kuambiwa vile na yeye hakupoteza muda akaangalia kwa njia ile ambapo lilikuja jina la JACKOB CHARLES taa za kichwa chake kilianza kupekua hili jina mara moja akagundua kwamba ni ‘bestman’ wake ambaye alikuwa ni Jakob, mara moja akanyanyua simu na kuweka sikioni ambapo kwa wakati huu sauti iliyosikika ilikuwa ni sauti ya Jakob mwenyewe ikiwa inaongea kwa furaha sana,,,,,,,,,
………..itaendelea
Ni mwanzo wa stori ya ‘’’’’’’secret document’’’’’’’’’’


Magazeti ya Tanzania March 10, 2017 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo




March 10 2017 Magazeti kurasa za mwanzo na mwisho kuanzia ya UdakuHardnews na Michezo 
























































New Posts

IJUE SCANIA P380[Mende]

Scania P380 Mende ni nini? Scania P380 ni mojawapo ya malori maarufu yaliyoundwa kwa nguvu na ufanisi wa hali ya juu, hasa kwa mazingira ya ...